Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Usalama Barabarani

𝐔𝐒𝐀𝐋𝐀𝐌𝐀 𝐁𝐀𝐑𝐀𝐁𝐀𝐑𝐀𝐍𝐈 𝐉𝐔𝐊𝐔𝐌𝐔 𝐋𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐀 𝐌𝐓𝐔 – 𝐒𝐀𝐉𝐄𝐍𝐓𝐈 𝐍𝐃𝐈𝐌𝐈𝐋𝐀

Picha
Na, Thadeo Gelema  Katika kipindi cha hivi karibuni, Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa lengo la kupunguza ajali na kuongeza uelewa wa matumizi sahihi ya barabara. Miongoni mwa askari wanaoendelea kufanya kazi kubwa ya utoaji elimu hiyo ni Sajenti David Ndimila ambaye amekuwa mstari wa mbele kuelimisha makundi mbalimbali ya watumiaji wa barabara ikiwemo madereva, bodaboda, abiria, wanafunzi pamoja na wananchi kwa ujumla. Kupitia kampeni mbalimbali za elimu, Sajenti Ndimila amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria za usalama barabarani, kuacha mwendokasi, kutumia usafiri salama, kuheshimu vivuko vya watembea kwa miguu pamoja na kutoa taarifa za makosa ya usalama barabarani. Miongoni mwa elimu alizozitoa ni pamoja na kuwataka madereva wa magari ya mizigo kuacha kuwaruhusu matingo kuendesha magari bila sifa za udereva, kuhimiza bodaboda kuheshimu misafara, kuwataka madereva kuchukua tahadhari wanapo...

𝐓𝐀𝐈𝐑𝐈 𝐂𝐇𝐀𝐊𝐀𝐕𝐔 𝐍𝐈 𝐂𝐇𝐀𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐉𝐀𝐋𝐈 𝐁𝐀𝐑𝐀𝐁𝐀𝐑𝐀𝐍𝐈

Picha
Na, Thadeo Gelema  Kuendesha gari lenye tairi zilizochakaa kumetajwa kuwa Moja ya sababu kubwa zinazosababisha ajali za barabarani. Picha: Sajenti Ndimila akitoa elimu kuhusu hatari ya tairi chakavu . Akitoa elimu hiyo Kwa madereva wa Magari ya mizigo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaelimisha  madereva kuacha Kuendesha Magari yenye tairi chakavu kuepuka ajali barabarani kwani tairi hizo huweza kupasuka ghafla na kupoteza uelekeo, kuteleza na kushindwa kusimama Kwa wakati pia kushindwa kustahimili kwenye barabara zenye mashimo na mawe Kisha kupelekea ajali barabarani  Picha: dereva akikumbushwa umuhimu wa ukaguzi wa tairi . Sajenti Ndimila amewataka madereva hao kukagua Magari hayo kabla ya kuanza safari na kubadilisha tairi chakavu pindi wanapozibaini ili kuzuia ajali zisizo za lazima wawapo barabarani. Picha: kwa ujumla Elimu ya usalama barabarani ikiendelea kutolewa kwa madereva ili kupunguza ajali na kulinda ...

𝐌𝐀𝐌𝐀 𝐖𝐀𝐉𝐀𝐖𝐀𝐙𝐈𝐓𝐎 𝐄𝐏𝐔𝐊𝐄𝐍𝐈 𝐒𝐀𝐅𝐀𝐑𝐈 𝐍𝐃𝐄𝐅𝐔 𝐌𝐊𝐈𝐊𝐀𝐑𝐈𝐁𝐈𝐀 𝐊𝐔𝐉𝐈𝐅𝐔𝐍𝐆𝐔𝐀

Picha
Na, Thadeo Gelema  Wanawake wajawazito wametakiwa kuepuka safari ndefu za mabasi wanapokuwa karibu kujifungua ili kujiepusha na madhara yanayoweza kuhatarisha maisha yao pamoja na watoto wanaowatarajia. Picha: Sajenti David Ndimila akitoa elimu kwa wasafiri kuhusu usalama wa mama wajawazito safarini. Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila , alipokuwa akizungumza na wasafiri ndani ya Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Shinyanga. Picha: Elimu ya usalama barabarani ikiendelea kutolewa kwa wajawazito katika Stendi Kuu ya Mabasi Shinyanga Sajenti Ndimila amesema wanawake wajawazito wanaosafiri wakiwa karibu kujifungua hukabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kujifungua ghafla ndani ya basi pasipo uwepo wa wakunga au vifaa tiba vya kumsaidia mama na mtoto. Picha: Wanawake wajawazito wakishauriwa kuepuka safari ndefu wanapokaribia kujifungua. Aidha, amesema mashimo yaliyopo barabarani pamoja na mitikisiko ya mabasi ...

𝐌𝐒𝐈𝐏𝐀𝐍𝐃𝐄 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐙𝐀 𝐌𝐈𝐙𝐈𝐆𝐎 𝐌𝐔𝐄𝐍𝐃𝐀𝐏𝐎 𝐌𝐈𝐍𝐀𝐃𝐀𝐍𝐈

Picha
Na, mwandishi wetu Shinyanga  Abiria wanaosafiri kwenda minadani wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuacha kupanda Bajaji za mizingo ili kuepukana na ajali za mara Kwa mara barabarani. Elimu hiyo imetolewa leo may 10, 2026 na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila katika barabara ya Old Shinyanga ambapo amewaeleza abiria kuwa Bajaji ya mizigo sio usafiri salama kwao na haina mazingira rafiki kulinda usalama wao hivyo kuacha tabia ya kupanda usafiri huo wa kubebea mizigo badala yake kutafuta usafiri unaoruhusiwa kubeba abiria. Sajenti Ndimila amewaeleza abiria hao kuwa kupanda bajaji ya mizigo ni hatari sana na inaweza kusababisha madhara makubwa kwao pindi ajali inapotokea. Aidha abiria hao wameaswa kujitambua na kuacha kurubuniwa kupanda katika usafiria huo kwani dereva wa chombo husika anaangalia maslahi binafsi na sio usalama wao. Picha: Sajenti David Ndimila akizungumza na wananchi kuhusu matumizi sahihi ya usafiri barabaran...

TOENI TAARIFA VITENDO VYA UKATILI SAFARINI

Picha
Abiria wa masafa marefu wamepatiwa elimu kuhusu kupaza sauti zao pindi wafanyiwapo au waonapo vitendo vya ukatili wa kijinsia vikitendeka ndani ya gari wawapo safarini Picha: Abiria wakikumbushwa umuhimu wa kuheshimiana, kulinda mipaka ya mwili na kutoa taarifa mapema pindi wanapoona au kufanyiwa ukatili. Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewataka abiria kutokukubaliana na vitendo hivyo kufanyika wakiwa safarini kama utolewaji wa lugha za udhalilishaji, kushikwa maungo  wanawake Kwa kisingizio Cha msongamano wa watu ndani ya gari, kupakatwa Kwa wanafunzi wa kike Kwa kisingizio Cha kukosa siti au kumdhalilisha mtu kulingana na umbo lake pia utolewaji wa lugha za vitisho. Picha: Abiria wa safari ndefu wakisikiliza elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia wakielekezwa na askari polisi. Aidha Sajenti Ndimila amewaeleza abiria kuwa mwili wa kila mtu ni wake, hakuna mtu mwenye haki ya kuugusa, kuuzungumzia au kumtumia ...

𝐋𝐈𝐏𝐄𝐍𝐈 𝐓𝐎𝐙𝐎 𝐙𝐀 𝐌𝐀𝐊𝐎𝐒𝐀 𝐁𝐀𝐑𝐀𝐁𝐀𝐑𝐀𝐍𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐓𝐈

Picha
Hii ni Thadeo Media  Madereva wa Magari Mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu utii wa Sheria bila shuruti Kwa kulipa tozo zinazotokana na makosa ya usalama barabarani Kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kuzuiwa na kulipa madeni Kwa lazima pindi tozo hizo zinapokuwa zimeongezeka baada ya siku saba kuisha. Picha: inaonesha askari wa usalama barabarani akifanya ukaguzi kwa dereva wa gari la mizigo lililosimama pembeni ya barabara. Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaelimisha madereva hao kuwa faida ya kulipa tozo hizo mapema inarahisisha usimamizi wa Sheria, inasaidia kuepuka usumbufu mara Kwa mara pia kuepuka adhabu Kali zaidi Picha: inaonesha askari wa usalama barabarani akiwa amesimama kando ya barabara akizungumza na dereva wa gari ndogo aina ya s Takix.  Aidha , Sajenti Ndimila amewataka wamikiki wa Magari kuwa na tabia ya kukagua Magari yao pindi wanapotoka kuwapa watu wengin...

𝐂𝐇𝐔𝐊𝐔𝐄𝐍𝐈 𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐕𝐈𝐕𝐔𝐊𝐎 𝐕𝐘𝐀 𝐑𝐄𝐋𝐈

Picha
 Na, Thadeo Gelema  Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu kuheshimu vivuko vya reli ili kuepuka ajali za mara Kwa mara. Picha: Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti David Ndimila, akitoa elimu kwa maafisa usafirishaji (bodaboda) kuhusu umuhimu wa kuheshimu vivuko vya reli. Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila katika kituo Cha Maafisa usafirishaji Cha Ally's star ambapo amewataka madereva hao kuheshimu vivuko vya reli Kwa kusimama na kujiridhisha hali ya kiusalama kabla ya kuchukua maamuzi ya kuvuka. Picha: Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda wakimsikiliza kwa makini Sajenti David Ndimila wakati wa mafunzo ya usalama barabarani katika kituo cha Ally’s Star, Shinyanga. Sajenti Ndimila amewaelimisha kwamba Treni inapaswa kupewa kipaumbele kwahiyo kila mmoja anawajibika kuheshimu vivuko hivyo kuepukana na a...

TUPINGE UKATAJI WA MABOMBA YA MOSHI KWENYE PIKIPIKI

Picha
𝙋𝙞𝙘𝙝𝙖: 𝙈𝙖𝙙𝙚𝙧𝙚𝙫𝙖 𝙬𝙖 𝙗𝙤𝙙𝙖𝙗𝙤𝙙𝙖 𝙬𝙖𝙠𝙞𝙨𝙞𝙠𝙞𝙡𝙞𝙯𝙖 𝙢𝙖𝙚𝙡𝙚𝙠𝙚𝙯𝙤 𝙠𝙪𝙩𝙤𝙠𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙖𝙨𝙠𝙖𝙧𝙞 𝙬𝙖 𝙪𝙨𝙖𝙡𝙖𝙢𝙖 𝙗𝙖𝙧𝙖𝙗𝙖𝙧𝙖𝙣𝙞 𝙠𝙪𝙝𝙪𝙨𝙪 𝙪𝙢𝙪𝙝𝙞𝙢𝙪 𝙬𝙖 𝙠𝙪𝙥𝙞𝙣𝙜𝙖 𝙠𝙚𝙡𝙚𝙡𝙚 𝙯𝙞𝙣𝙖𝙯𝙤𝙩𝙤𝙠𝙖𝙣𝙖 𝙣𝙖 𝙢𝙖𝙗𝙤𝙢𝙗𝙖 𝙮𝙖 𝙢𝙤𝙨𝙝𝙞 𝙮𝙖𝙡𝙞𝙮𝙤𝙠𝙖𝙩𝙬𝙖 𝙠𝙬𝙚𝙣𝙮𝙚 𝙥𝙞𝙠𝙞𝙥𝙞𝙠𝙞. 𝙃𝙞𝙞 𝙣𝙞 𝙏𝙝𝙖𝙙𝙚𝙤 𝙈𝙚𝙙𝙞𝙖 𝗟𝗲𝗼 𝗠𝗮𝗿𝗰𝗵 𝟬𝟵, 𝟮𝟬𝟮𝟲 𝗠𝗮𝗱𝗲𝗿𝗲𝘃𝗮 𝘄𝗮 𝗽𝗶𝗸𝗶𝗽𝗶𝗸𝗶 𝘇𝗮 𝗸𝘂𝗯𝗲𝗯𝗮 𝗮𝗯𝗶𝗿𝗶𝗮, 𝗺𝗮𝗮𝗿𝘂𝗳𝘂 𝗸𝗮𝗺𝗮 𝗯𝗼𝗱𝗮𝗯𝗼𝗱𝗮, 𝗺𝗸𝗼𝗮𝗻𝗶 𝗦𝗵𝗶𝗻𝘆𝗮𝗻𝗴𝗮 𝘄𝗮𝗺𝗲𝗽𝗲𝘄𝗮 𝗲𝗹𝗶𝗺𝘂 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗵𝗮𝗺𝗮𝘀𝗶𝘀𝗵𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗽𝗶𝗻𝗴𝗮 𝘃𝗶𝘁𝗲𝗻𝗱𝗼 𝘃𝘆𝗮 𝘂𝗵𝗮𝗿𝗶𝗯𝗶𝗳𝘂 𝗮𝘂 𝘂𝗸𝗮𝘁𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝗺𝗮𝗯𝗼𝗺𝗯𝗮 𝘆𝗮 𝗺𝗼𝘀𝗵𝗶 (𝗲𝘅𝗵𝗮𝘂𝘀𝘁) 𝗸𝘄𝗲𝗻𝘆𝗲 𝗽𝗶𝗸𝗶𝗽𝗶𝗸𝗶. 𝗩𝗶𝘁𝗲𝗻𝗱𝗼 𝗵𝗶𝘃𝘆𝗼 𝗵𝘂𝘀𝗮𝗯𝗮𝗯𝗶𝘀𝗵𝗮 𝗸𝗲𝗹𝗲𝗹𝗲 𝗻𝗮 𝗺𝗶𝗹𝗶𝗽𝘂𝗸𝗼 𝗺𝗶𝗸𝗮𝗹𝗶 𝘆𝗮 𝘀𝗮𝘂𝘁𝗶 𝗯𝗮𝗿𝗮𝗯𝗮𝗿𝗮𝗻𝗶 𝗻𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗶𝘁𝗮𝗮 𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶𝗺𝗯𝗮𝗹𝗶. 𝗔𝗸𝗶𝘁𝗼𝗮 𝗲𝗹𝗶𝗺𝘂 𝗵𝗶𝘆𝗼, 𝗔𝘀...

POLISI DAR WAKAMATA WEVYE MILIO MIKALI YA PIKIPIKI NA MAGARI

Picha
  Picha hii ni ya mfano kwa madhumuni ya kuonesha tukio husika na sio tukio halisi lililotokea wakati wa kukamatwa kwa watuhumiwa. Chanzo: Thadeo Media Library Photo . Na, Thadeo Gelema  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha vyombo vya moto kwa kutoa milio mikali ya milipuko kinyume cha sheria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi iliyotolewa Machi 06, 2026, watuhumiwa hao wanadaiwa kuendesha magari na pikipiki zenye kelele kali zinazofanana na milipuko, hali inayosababisha usumbufu na hofu kwa wananchi pamoja na kukiuka Sheria ya Usalama Barabarani. Watuhumiwa waliokamatwa ni Abdallah Masumbuko mkazi wa Tabata, Julius Dismas mkazi wa Mwananyamala, Salehe Ally mkazi wa Kijitonyama na Mohamed Rashid mkazi wa Magomeni. Wote wanashikiliwa na Polisi huku hatua zaidi za kisheria zikiendelea kuchukuliwa dhidi yao. Kwa ujumla, Jeshi la Polisi limewahimiza watumiaji wote wa barab...

MSIVUKE BARABARA MUONAPO MAGARI YA DHARURA YAKIPITA

Picha
Picha: Sajenti David Ndimila akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Nhelegani, Shinyanga Hii ni Thadeo Media Leo March 03, 2026 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nhelegani iliyopo mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kuepuka kuvuka barabara wanapoona magari ya dharura yakipita. Akitoa elimu hiyo, askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, amesema kuwa magari ya dharura ni yale yanayotoa huduma za kuokoa maisha na kulinda usalama wa umma. Magari hayo ni pamoja na ya kubebea wagonjwa, zimamoto na polisi. Amefafanua kuwa magari ya dharura hupaswa kuwa na ving’ora au taa za bluu na nyekundu zinazomulika ili yapatiwe kipaumbele barabarani. Aidha, Sajenti Ndimila amewasisitiza wanafunzi hao kuongeza umakini wanapotaka kuvuka barabara. Hata wanapokuwa kwenye kivuko cha watembea kwa miguu, wanapaswa kutoa kipaumbele kwa magari ya dharura kupita kwanza. Picha: Sajenti David Ndimila akitoa elimu ya usalama bara...

TUMIA IPASAVYO ALAMA YA PEMBETATU

Picha
  Picha: Sajenti David Ndimila akiwafundisha madereva juu ya matumizi sahihi ya alama ya pembetatu kuzuia aja Leo March 01, 2026  Madereva wa magari ya kubeba abiria wamekumbushwa umuhimu wa kubeba na kutumia ipasavyo alama ya pembetatu ya tahadhari (reflective triangle) pindi gari linapopata hitilafu barabarani, ili kuzuia ajali na kulinda usalama wa watumiaji wengine wa barabara. Akizungumza na madereva hao, Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, amesema alama hiyo ni muhimu kwa kuwaonya madereva wengine kuhusu uwepo wa gari lililoharibika, ajali au hatari iliyo mbele yao. Ameeleza kuwa alama ya pembetatu inapaswa kuwekwa nyuma ya gari lililopata hitilafu na wakati mwingine mbele, kulingana na mazingira ya barabara, ili ionekane kwa urahisi mchana na usiku. Kwa mujibu wa Sajenti Ndimila, alama hiyo inatakiwa kuwekwa umbali wa mita 50 hadi 100 kutoka lilipo gari lililoharibika. Umbali wa mita 100 unapendekezwa katika barabara za mwen...

CHUKUA TAHADHALI KABLA YA KULIPITA GARI LINGINE

Picha
PICHA: Sajenti David Ndimila akitoa elimu ya usalama kwa madereva kuhusu namna sahihi ya kulipita gari barabarani .    Hii ni Thadeo media Leo February 26, 2026 Madereva wa magari makubwa yanayokwenda masafa marefu wamepatiwa elimu ya namna ya kujiepusha na ajali wanapotaka kuyapita magari mengine barabarani. Elimu hiyo imetolewa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, ambaye amewataka madereva kujiridhisha kuwa hakuna hatari kwa watumiaji wengine wa barabara kabla ya kufanya uamuzi wa kulipita gari lililo mbele yao. Amesisitiza kuwa kabla ya kulipita gari la mbele, dereva anatakiwa kuacha nafasi ya kutosha kati ya gari analoliendesha na lile lililo mbele yake ili aweze kuona kwa urahisi magari yanayokuja kutoka upande wa mbele, na hivyo kufanya maamuzi sahihi na salama . PICHA: Mbali mbali Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, akitoa elimu kwa madereva wa magari makubwa yanayosafiri masaf...

RASIMISHENI NAMBA ZA USAJILI ZA VYOMBO VYA MOTO.

Picha
Picha: Sajenti David Ndimila wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga akitoa elimu kwa dereva    Leo February 23, 2026 Madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kufanya urasimishaji wa namba za usajili za vyombo hivyo pasipo shuruti mara baada ya kibali Cha muda mfupi kuisha. Akitoa elimu hiyo Kwa madereva wa vyombo vya moto Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaeleza kuwa kuendesha vyombo vya moto Kwa kutumia namba ya chasi (chasiss number) bila namba ya usajili ni kosa kisheria mara baada ya muda wa kibali hicho Cha muda mfupi kuisha. Sajenti Ndimila amewataka madereva hao kujisimamia na kutekeleza takwa la kisheria bila shuruti pindi wanapotoa vyombo hivyo bandarini au kuvinunua vikiwa na namba ya chasi (chassis number) Picha: Sajenti David Ndimila wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga akitoa elimu kwa dereva, huku chombo cha moto kikiwa vimeegeshwa pembeni ya barabara wakati Mmiliki wake wakimsikili...