Abiria wa masafa marefu wamepatiwa elimu kuhusu kupaza sauti zao pindi wafanyiwapo au waonapo vitendo vya ukatili wa kijinsia vikitendeka ndani ya gari wawapo safarini |
| Picha: Abiria wakikumbushwa umuhimu wa kuheshimiana, kulinda mipaka ya mwili na kutoa taarifa mapema pindi wanapoona au kufanyiwa ukatili. |
Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewataka abiria kutokukubaliana na vitendo hivyo kufanyika wakiwa safarini kama utolewaji wa lugha za udhalilishaji, kushikwa maungo wanawake Kwa kisingizio Cha msongamano wa watu ndani ya gari, kupakatwa Kwa wanafunzi wa kike Kwa kisingizio Cha kukosa siti au kumdhalilisha mtu kulingana na umbo lake pia utolewaji wa lugha za vitisho.
 |
| Picha: Abiria wa safari ndefu wakisikiliza elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia wakielekezwa na askari polisi. |
Aidha Sajenti Ndimila amewaeleza abiria kuwa mwili wa kila mtu ni wake, hakuna mtu mwenye haki ya kuugusa, kuuzungumzia au kumtumia kingono bila ruhusa yake kamili.
 |
| Picha: Sajenti wa usalama barabarani akizungumza na abiria kuhusu haki zao na umuhimu wa kuripoti vitendo vya ukatili. |
Abiria wamesisitizwa kuwa kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie Kwa kupaza sauti zao na kuzuia vitendo hivyo Kwa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
 |
| Picha: Abiria wakihamasishwa kuwa walinzi wa wenzao kwa kupaza sauti na kutoa taarifa dhidi ya ukatili wa kijinsia. |
Kwa ujumla, elimu hii inalenga kuwajengea abiria ujasiri wa kukataa na kuripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia, huku ikisisitiza wajibu wa kila mmoja kulinda usalama na heshima ya wengine safarini.
Maoni
Chapisha Maoni