𝐊𝐈𝐃𝐀𝐓𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐍𝐍𝐄 𝐀𝐅𝐀𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐃𝐔𝐍𝐈𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀
Shinyanga Mwanafunzi wa kidato cha nne anayefahamika kwa jina la Rebecka Boniphace Maganga (1 7), aliyekuwa akisoma katika Shule ya Sekondari Old Shinyanga, amefariki dunia kwa tuhuma za kujinyonga ndani ya chumba alichokuwa akiishi. Tukio hilo lilitokea Aprili 27, 2026 majira ya saa saba mchana katika eneo la Old Shinyanga, ambapo inadaiwa mwanafunzi huyo alijinyonga kwa kutumia mkanda wa sketi ya shule. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi Janeth Magomi, jeshi la polisi lilipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa mlezi wa marehemu, Mashala Piter (56), ambaye aligundua tukio hilo. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa tukio hilo linaweza kuhusishwa na msongo wa mawazo, baada ya mwanafunzi huyo kurejeshwa nyumbani na mwalimu wake akiwa na mzazi wake kufuatia kutohudhuria masomo kwa muda wa wiki mbili bila taarifa. Mwenyekiti wa kitongoji cha Senyenge , kijiji cha Old Shinyanga, Benjamin Andrew, alisema walipokea taarifa za tukio hilo maj...