Michezo
Kipigo Cha Silver Strikers Chamaliza Ndoto za Folz Yanga SC Na Thadeo Gelema Dar es Salaam , 18 Oktoba 2025 — Klabu ya Young Africans SC (Yanga) imetangaza rasmi kuachana na kocha wao Romain Folz kufuatia kipigo cha 1–0 kutoka kwa Silver Strikers ya Malawi katika mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa 18 Oktoba 2025. Uamuzi huo umetajwa kuwa sehemu ya hatua za dharura zilizochukuliwa na uongozi wa Yanga baada ya matokeo yasiyoridhisha katika mechi za kimataifa, huku mashabiki wengi wakionyesha kutoridhishwa na mwelekeo wa timu chini ya Folz. Mabedi Achukua Mikoba Baada ya tangazo hilo, kocha msaidizi Patrick Mabedi ametangazwa rasmi kuwa kocha wa mpito huku uongozi wa klabu ukiendelea kutafuta kocha mpya wa kudumu. Mabedi atakuwa na jukumu la kuhakikisha timu inarejea kwenye ushindi na kuimarisha morali ya wachezaji kabla ya mechi za marudiano. Folz na Yanga: Mwisho Usiotarajiwa Romain Folz alijiunga na Yanga mnamo Julai 2025 na alitarajiwa kuendeleza ma...