HAKUNA MGONJWA WA UVIKO-19 NCHINI – MHE. MCHENGERWA
Hii ni Thadeo Media – WAF, Dar es Salaam. Wizara ya Afya imewataka wananchi kuendela kuchukua tahadhari na kufuatilia ushauri wa kitaalam ili kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kama ilivyoelezwa katika taarifa kwa umma ya Mganga Mkuu wa Serikali hivi karibuni. Hayo yamebainishwa leo Februari 27, 2026 Jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa alipofanya ziara ya kimakakati katika hospitali ya Rufaa Mkoa Amana kwa lengo la kukagua utolewaji wa huduma za afya pamoja na maendeleo ya uboreshaji wa miundombinu ya hospitali hiyo. Aidha amesema, Serikali bado inaendelea kufuatilia kwa ukaribu juu ya mienendo ya magonjwa mbalimbali kama kipindu pindu, Dengue na UVIKO-19 hususani katika kipindi hiki cha mvua huku akisistiza kwamba hakuna kisa chochote UVIKO, cha mgonjwa aliyelazwa katika hospitali nchini. “Napenda kuwahakikishia wananchi na Watanzania wote Serikali yenu ipo makini na inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa maambukizi ya UVIKO-19 nchini na kimataifa,...