RAIS WA ST. JOSEPH COLLEGE ANGARA UZINDUZI WA JUKWAA LA VIJANA SHINYANGA

Picha inamuonyesha Vicent Chacha, Rais wa Chuo cha St. Joseph College Shinyanga, akiwa ameshere kwenye WhatsApp status yake leo, Februari 21, 2026, akionyesha ushirikiano wake na serikali na kuonyesha kuwa amewasilisha ombi la wanafunzi wa vyuo vya kati kuhusu mgawanyo sawa wa mikopo ya elimu.



         
Na Thadeo gelema

Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha St. Joseph College Shinyanga, Vicent Chacha, ameitumia nafasi yake kuzungumza mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana kuwasilisha ombi la mgawanyo sawa wa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya kati, akisisitiza kuwa nao ni Watanzania wenye haki ya kunufaika na fursa za kiuchumi.

Vicent alisema kuwa mikopo hiyo itasaidia wanafunzi wa vyuo vya kati kumudu gharama za masomo na kujenga msingi imara wa maisha yao ya baadaye. Aliongeza kuwa kusikilizwa kwa hoja hiyo ni hatua kubwa kwa wanafunzi wengi waliokuwa wakikosa sauti ya kuwasilisha changamoto zao.

Hatua hiyo imekuja sambamba na wito wa Waziri kwa vijana kuacha kuwa watazamaji wa uchumi na badala yake washiriki kikamilifu kwa kutumia fursa za mikopo, mafunzo ya ujuzi na teknolojia zinazotolewa na Serikali. Huku akiahidi waziri kulifikisha bodi ya mikopo na litafavyiwa kazi

Picha: Vicent Chacha, Rais wa St. Joseph College Shinyanga, akiwa eneo la tukio!



Vicent ameeleza kuwa kupewa nafasi ya kuzungumza mbele ya kiongozi wa kitaifa ni heshima kubwa na ushahidi kuwa vijana wakiamua kuthubutu wanaweza kuwa sehemu ya maamuzi muhimu ya maendeleo.

Kwa ujumla, Hatua ya Rais huyo wa wanafunzi imeonekana kuwa chachu kwa vijana wengine kujiamini, kusimamia ndoto zao na kutumia majukwaa wanayopata kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Maoni

Chapisha Maoni