🇲🇦 Morocco Watwaa Taji la Tatu: “Pamoja Katika Historia, Pamoja Katika Heshima” – Morocco na Madagascar Waandika Historia ya CHAN 2024 Thadeo Media | Michezo & Burudani | Agosti 30, 2025 Morocco Watawala Kasarani Nairobi, Agosti 30, 2025 – Morocco wameandika sura mpya ya soka barani Afrika baada ya kuifunga Madagascar 3-2 kwenye fainali ya CHAN 2024, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Moi International Sports Centre, Kasarani. Ushindi huu unawakilisha taji lao la tatu, na kuashiria nguvu na uhodari wa mabingwa hawa wenye historia. Madagascar walionesha ushindani mkubwa na moyo wa ajabu, wakitupa somo la kuthubutu na kuonyesha dark horse wa mashindano. Matokeo ya Mechi Timu Mabao Wachezaji Waliofunga Madagascar 2 Félicité Manouhantzua (9'), Toky Rakotondraibe (68') Morocco 3 Youssef Mehri (27'), Oussama Lamlioui (44', 80') Muhtasari: Madagascar waliongoza mapema, lakini Morocco walijibu kwa nguvu na Lamlioui kufunga mabao mawili muhimu nakuwa mfungaji ...