GARAGE FC vs ST. JOSEPH’S COLLEGE FC: IJUMAA HII, Baada ya Mitihani, Sasa Ni Muda wa Burudani – Ijumaa Hii Laini Polisi Shinyanga, Julai 31, 2025 Na: Thadeo Media Baada ya kumaliza mitihani ya mwisho kwa mafanikio makubwa, wanafunzi wa St. Joseph’s College of Shinyanga (STJOSO) sasa wanajiandaa kwa burudani kabambe kupitia tukio maalum la michezo litakalowakutanisha na Garage FC kwenye mechi ya kirafiki yenye mvuto wa kipekee. Mechi hiyo itachezwa Ijumaa hii, Agosti 1, 2025, kuanzia saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Laini Polisi – Shinyanga. Ni fursa adimu kwa wanafunzi, wakufunzi na wadau wa elimu kuungana pamoja kusherehekea mafanikio ya kitaaluma kupitia ushindani wa kiwanjani. “Mchezo huu si tu burudani, bali pia ni njia ya kujenga mshikamano wa kijamii na kupunguza msongo wa mawazo baada ya mitihani,” amesema Waziri wa Habari wa STJOSO. 👉 Kila Mtu Anakaribishwa: Wanafunzi wa chuo, walimu, wahitimu, marafiki na wadau wa michezo – mnaombwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia ...