Na, Thadeo Gelema Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 20, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni: Mhe. Abdi Shaaban Kagomba (Kutoka Kanda ya Dodoma) Mhe. Yohane Bokobora Masara (Kutoka Kanda ya Arusha) Mhe. Immaculata Kajetan Banzi (Kutoka Kanda ya Kagera) Mhe. Rabia Hussein Mohamed (Kutoka Mahakama Kuu ya Zanzibar) Mhe. Cyprian Phocas Mkeha (Kutoka Divisheni ya Biashara, DSM) Mhe. Yose Joseph Mlyambina (Kutoka Divisheni ya Kazi, DSM) kwa ujumla, uapisho wa Majaji hao wateule utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika taasisi mbalimbali za umma nchini . Na, Thadeo Gelema Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo Ijumaa, Mei 22, 2026, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo unajumuisha viongozi wafuatao waliopangiwa kusimamia bodi hizo muhimu: Orodha ya Walioteuliwa na Taasisi Zao: Ludovick James Nduhiye – Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa. Dkt. Irene Charles Isaka – Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Jamhuri Joseph Ngelime – Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF). kwa ujumla , Ufanisi Katika Utendaji Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na Millard Ayo UPDATES, uteuzi huu wa viongozi unatarajiwa kuongeza kasi ya kiutendaji, uwajibikaji, pamoja na kuboresha mifumo ya...
Na, Thadeo Gelema DODOMA : Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa rasmi kwa umma likitaka wananchi kupuuza picha mjongeo (video) inayosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, likieleza kuwa taarifa hizo ni za uongo na uzushi wenye lengo la kuzua taharuki. Video hiyo inayosambazwa inaonyesha picha ya maiti ikiambatana na maandishi yanayodai kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyetekwa, kubakwa, kuuawa na kisha mwili wake kutelekezwa chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) mkoani Dodoma Huku wengine wakizidi kuandika kulingana na wanayo amini wao. Ufafanuzi wa Jeshi la Polisi Chanzo cha Picha na Taarifa: Polisi Tanzania on Instagram Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumamosi, Mei 23, 2026, na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Mkuu ya Polisi Dodoma, imesisitizwa kuwa: Hakuna tukio kama hilo lililotokea mkoani Dodoma wala katika maeneo mengine yoyote nchini Tanzania. Hata kama ingekuwa ni tukio la kweli lililotokea mahali popote, picha na video za nam...
Maoni
Chapisha Maoni