𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀


Na, Thadeo Gelema 

DODOMA: Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa rasmi kwa umma likitaka wananchi kupuuza picha mjongeo (video) inayosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, likieleza kuwa taarifa hizo ni za uongo na uzushi wenye lengo la kuzua taharuki.

​Video hiyo inayosambazwa inaonyesha picha ya maiti ikiambatana na maandishi yanayodai kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyetekwa, kubakwa, kuuawa na kisha mwili wake kutelekezwa chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) mkoani Dodoma Huku wengine wakizidi kuandika kulingana na wanayo amini wao.

Ufafanuzi wa Jeshi la Polisi

Chanzo cha Picha na Taarifa: Polisi Tanzania on Instagram 

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumamosi, Mei 23, 2026, na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Mkuu ya Polisi Dodoma, imesisitizwa kuwa:

​Hakuna tukio kama hilo lililotokea mkoani Dodoma wala katika maeneo mengine yoyote nchini Tanzania.

​Hata kama ingekuwa ni tukio la kweli lililotokea mahali popote, picha na video za namna hiyo hazistahili kabisa kusambazwa mitandaoni kwa misingi ya utu na maadili.

Uchunguzi na onyo

​Jeshi la Polisi limebainisha kuwa tayari linaendelea kuwafuatilia kwa karibu watu wote waliohusika kuchukua picha hiyo na kuitengenezea maelezo ya uongo.

Aidha, limetoa wito mkali kwa wananchi wote walionayo kwenye simu zao au wanaotumiwa video hiyo, kuacha mara moja kuendelea kuisambaza ili kuepuka kuingia kwenye matatizo ya kisheria.

Kwa ujumla, Jeshi la Polisi linawasihi wananchi kuwa makini na taarifa wanazozipokea na kuzisambaza mtandaoni. Ili kulinda amani na kuzuia taharuki zisizo na msingi, ni muhimu kujiridhisha na vyanzo rasmi vya habari kabla ya kushiriki picha au video zozote kwenye mitandao ya kijamii.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI