Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Habari

𝐁𝐈. 𝐒𝐔𝐙𝐀𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐆𝐔𝐅𝐔𝐋𝐈 𝐀𝐅𝐀𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐃𝐔𝐍𝐈𝐀

Picha
Na, Thadeo Gelema  Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, Suzana Magufuli amefariki dunia leo Mei 25, 2026, Chato Mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mrefu. Kwa mujibu wa @AyoTV Akizungumza kwa njia ya simu, Mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli amethibitisha kutokea kwa msiba huo akieleza kuwa Bibi Suzana amefariki saa 1 usiku Nyumbani kwake Chato. “Bibi yetu (Suzana Mussa) amefariki saa moja nyumbani kwake Chato baada ya kuugua kwa muda mrefu, taratibu za msiba familia itawajulisha, Bwana ametoa na Bwana ametwaa” Jesca.

𝐇𝐔𝐊𝐔𝐌𝐔: 𝐌𝐈𝐀𝐊𝐀 80 𝐉𝐄𝐋𝐀,𝐕𝐈𝐁𝐎𝐊𝐎 6 𝐍𝐀 𝐅𝐈𝐃𝐈𝐀 𝐌𝐈𝐋𝐈𝐎𝐍𝐈 26

Picha
Na, Mwandishi wetu  ​ KATAVI : Mahakama ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha jumla ya miaka 80 jela Bw. Jofrey Musa Masanja (27), baada ya kupatikana na hatia ya makosa sita (06) ya unyang'anyi wa kutumia silaha na kujeruhi. ​Mbali na kifungo hicho cha miaka 80 jela, Mahakama pia imempa adhabu ya kuchapwa viboko sita (06), kulipa fidia ya jumla ya shilingi milioni 10 (10,000,000 TZS) kwa majeruhi wote, pamoja na kurudisha kiasi cha shilingi milioni 16 (16,000,000 TZS) kilichoibiwa. ​Ukatili Aliotenda kwa Nyakati Tofauti ​Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Sylivester Makombe, ameeleza kuwa mshitakiwa alitenda makosa hayo ya kikatili katika Kijiji cha Vikonge wilayani Tanganyika kwa nyakati tatu tofauti mnamo Novemba 2024: ​Novemba 19, 2024: Alimvamia na kumfunga kamba mwili mzima mwananchi John Burunda, kisha kumshambulia na kumuibia kiasi cha shilingi 60,000. ​Novemba 22 na Novemba 26, 2024: Akitumia silaha yenye ncha kali (kisu) na fi...

𝐓𝐔𝐍𝐃𝐔 𝐋𝐈𝐒𝐒𝐔; 𝐊𝐔𝐔𝐆𝐔𝐑𝐔𝐌𝐀 𝐌𝐀𝐇𝐀𝐊𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈 𝐊𝐄𝐒𝐇𝐎

Picha
Na, Thadeo Gelema  Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, anatarajiwa kufikishwa Mahakamani kesho Jumatatu, Mei 25, 2026. Hatua hiyo inakuja kwa ajili ya kusikiliza maombi ya kuunganishwa kwake katika kesi kubwa inayohusu usimamizi na umiliki wa mali za chama hicho. ​Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, shauri hilo litasikilizwa mbele ya Jaji Ngunyale, ambapo Lissu atahudhuria akisimama katika nafasi yake ya uongozi wa juu ndani ya chama. ​ Saa ya Mgogoro na Mapambano ya Kisheria ​Kesi hii inahusiana kwa karibu na mgogoro wa ndani wa mali za CHADEMA pamoja na uhusiano wa kisheria wa viongozi wake wakuu katika mchakato mzima wa usimamizi wa rasilimali hizo. ​Usikilizwaji wa kesi hiyo unatarajiwa kuanza mapema asubuhi:   HOJA MAHAKAMANI: Mashauri yanatarajiwa kuanza majira ya saa 2:45 asubuhi, huku pande zote mbili za utetezi na mashitaka zikitajiwa kuwasilisha hoja zao ...

𝐌𝐖𝐈𝐍𝐘𝐈; 𝐒𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐈𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐌𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐔𝐑𝐀𝐈𝐒

Picha
Na, Thadeo Gelema  ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesitisha rasmi mijadala inayohusu kuongeza muda wa urais wake zaidi ya miaka 10 iliyowekwa kikatiba, akisisitiza kuwa hana nia hiyo na kwamba mjadala huo hauna tija yoyote. Dkt. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo, Mei 23, 2026, alipofungua Jukwaa la Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi za Umma katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Airport, Mkoani Mkoa wa Mjini Magharibi. ​Alieleza kuwa viongozi walioapa kulinda Katiba wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, na kubainisha kuwa kipindi kilichobaki cha uongozi wake kitalenga utekelezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo na sio mijadala isiyo na tija. ​Mashirika ya Umma Kupunguziwa Ruzuku ​Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Mwinyi ametoa onyo kali kwa mashirika ya umma yanayoendelea kutegemea ruzuku na mishahara kutoka serikalini badala ya kujiendesha kwa tija na faida. ​"Serikali haitakuwa tayari kuendelea kubeba mzigo wa ...

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀

Picha
Na, Thadeo Gelema  DODOMA : Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa rasmi kwa umma likitaka wananchi kupuuza picha mjongeo (video) inayosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, likieleza kuwa taarifa hizo ni za uongo na uzushi wenye lengo la kuzua taharuki. ​Video hiyo inayosambazwa inaonyesha picha ya maiti ikiambatana na maandishi yanayodai kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) aliyetekwa, kubakwa, kuuawa na kisha mwili wake kutelekezwa chumba cha kuhifadhia maiti (mortuary) mkoani Dodoma Huku wengine wakizidi kuandika kulingana na wanayo amini wao. ​ Ufafanuzi wa Jeshi la Polisi Chanzo cha Picha na Taarifa:  Polisi Tanzania on Instagram  Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumamosi, Mei 23, 2026, na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Mkuu ya Polisi Dodoma, imesisitizwa kuwa: ​Hakuna tukio kama hilo lililotokea mkoani Dodoma wala katika maeneo mengine yoyote nchini Tanzania. ​Hata kama ingekuwa ni tukio la kweli lililotokea mahali popote, picha na video za nam...

𝐌𝐔𝐅𝐓𝐈 𝐌𝐊𝐔𝐔 𝐓𝐙: 𝐒𝐈𝐊𝐔𝐊𝐔𝐔 𝐘𝐀 𝐄𝐈𝐃 𝐀𝐋-𝐀𝐃𝐇𝐀 𝐍𝐈 𝐉𝐔𝐌𝐀𝐓𝐀𝐍𝐎, 𝐌𝐄𝐈 27

Picha
  Na, Thadeo Gelema  Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Bin Zuber Ally, amewatangazia Waislamu na wananchi wote kwa ujumla kuwa Sikukuu ya Eid Al-Adha mwaka huu itakuwa siku ya Jumatano, Mei 27, 2026. ​Ujumbe Kutoka Makkah ​Akiongea akiwa nchini Saudi Arabia katika mji mtukufu wa Makkah, Sheikh Zubeir amewaombea heri waumini waliopo kwenye ibada ya Hijja na wale waliobaki nyumbani: ​ "Namuomba Mungu atukamilishie Hijja yetu, tupate Hijja iliyokamilika na wale wenzetu ambao hawakupata bahati ya kuja katika mawanja haya, waweze kutekeleza Ibada nyingine nyumbani na Mungu awalete mwaka ujao hapa katika mawanja ya Makkah." ​Sherehe za Kitaifa Kufanyika Dar es Salaam ​Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na Millard Ayo, Sherehe za Eid Al-Adha Kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika mkoani Dar es Salaam. ​Swala ya Eid itasaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI BAKWATA Makao Mkuu, uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 1:30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Ei...

𝐇𝐎𝐍𝐆𝐄𝐑𝐀 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐔𝐃𝐇𝐈𝐁𝐈𝐓𝐈 𝐔𝐇𝐀𝐋𝐈𝐅𝐔 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐈𝐌𝐀𝐋𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐀𝐌𝐀𝐍𝐈

Picha
Na, mwandishi wetu Shinyanga  Kamati ya Maridhiano na Amani Mkoa wa Shinyanga imelipongeza Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga chini ya uongozi wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi , kwa juhudi zake za kudhibiti vitendo vya uhalifu na kuimarisha hali ya usalama pamoja na amani kwa wananchi. Picha: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi akizungumza kuhusu juhudi za Jeshi la Polisi katika kudhibiti vitendo vya uhalifu na kuimarisha usalama wa wananchi. Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano, Amani, Mila na Desturi Mkoa wa Shinyanga, Shehe Balilusa Khamis, alipokuwa akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo. Katika tukio hilo, alikuwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa dini, wazee wa kimila pamoja na Mkuu wa Machifu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha: Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano, Amani, Mila na Desturi Mkoa wa Shinyanga, Shehe Balilusa Khamis akilipon...

𝐊𝐈𝐊𝐀𝐀𝐍𝐆𝐎𝐍𝐈 𝐊𝐔𝐋𝐀𝐖𝐈𝐓𝐈 𝐌𝐓𝐎𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐀𝐊𝐀 6

Picha
 Na,Thadeo Gelema  Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Kesi Juma Ibrahim, Miaka 22 , Mkulima na mkazi wa Kifuleta, Chalinze kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka 6 (Jina linahifadhiwa). Mnamo Mei 17, 2026 majira ya saa 7:00 mchana huko katika Kijiji cha Kifuleta, Kata ya Kimange, Chalinze mtuhumiwa alimlaghai mtoto huyo ambaye ni jirani yake na kumuingiza chumbani kwake kisha kumfanyia kitendo hicho. Baada ya wazazi kugundua kuwa mtoto amefanyiwa kitendo hicho waliripoti kituo cha Polisi Mbwewe ambapo jitihada zilifanyika na mtuhumiwa huyo kukamatwa. Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea na upelelezi na mara utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani. Kwa ujumla , Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea na upelelezi wa tukio hilo, huku likisisitiza kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.

MAZISHI YA MARTINE KUFANYIKA LEO SHINYANGA

Picha
Mazishi ya aliyekuwa Mpiga Picha wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, marehemu Boaz Martine, yanatarajiwa kufanyika kesho Alhamisi Mei 21, 2026 katika makaburi ya familia yaliyopo Mwawaza, Manispaa ya Shinyanga. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, David Lyamongi, ibada ya kumuombea marehemu itaongozwa na Mashahidi wa Yehova kuanzia saa 7:00 mchana nyumbani kwa marehemu nyuma ya Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kitangili, Manispaa ya Shinyanga. Baada ya ibada na salamu za rambirambi, mwili wa marehemu utapelekwa katika makaburi ya familia yaliyopo Mwawaza kwa ajili ya mazishi yatakayoanza majira ya saa 9:00 alasiri. Marehemu Boaz Martine alifariki dunia Mei 19, 2026 kufuatia ajali ya barabarani iliyotokea katika eneo la Samuye mkoani Shinyanga, ajali iliyohusisha gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Akizungumza na waandis...

𝐀𝐉𝐀𝐋𝐈 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀: 𝐌𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐀𝐅𝐀𝐑𝐈𝐊𝐈, 𝐖𝐀𝐀𝐍𝐃𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝐌𝐀𝐉𝐄𝐑𝐔𝐇𝐈

Picha
Shinyanga Mpiga picha wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Boaz Martine amefariki dunia huku waandishi wa habari Frank Mshana wa ITV/Radio One na Johnson James wakiwa miongoni mwa watu saba waliojeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea Mei 19, 2026 katika Kata ya Samuye, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga. Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba T.210 EDB na Toyota Land Cruiser Hardtop lenye namba DFPA 8920 mali ya shirika la KOICA, lililokuwa limebeba waandishi wa habari pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 20, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Harrier aliyekuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari, hali iliyosababisha kugongana na Land Cruiser hiyo na kutumbukia mtaroni. Mbali na Frank Mshana na Johnson James afisa habari ofisi ya mkuu wa Mkoa, majeruhi we...

𝐌𝐀𝐌𝐀 𝐊𝐔𝐔𝐏𝐈𝐆𝐀 𝐌𝐖𝐈𝐍𝐆𝐈, 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐍𝐈𝐒𝐇𝐀𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐍𝐘𝐔𝐊𝐋𝐈𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀

Picha
Na, Thadeo Gelema  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali ambapo atashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA) , Kigali nchini Rwanda Mei 19, 2026. Mkutano huo wa Kimataifa unawakutanisha pia wataalamu wa nishati, wawekezaji na mashirika ya kimataifa, ambapo utajadili matumizi ya nishati ya nyuklia kwa maendeleo ya Bara la Afrika. Mkutano huo pia unalenga kujadili namna bora ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme Afrika, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kusaidia maendeleo ya viwanda, kukuza ubunifu wa teknolojia za nishati ya nyuklia pamoja na kuvutia wawekezaji katika miradi ya nishati. Kwa ujumla , Mkutano huo unatajwa kuwa hatua muhimu kwa Afrika katika kutafuta suluhisho la nishati safi, maendeleo ya teknolojia na kuongeza uwekezaji utakaosaidia kukuza uchumi na viwanda barani humo.

𝐖𝐀𝐍𝐍𝐄 𝐊𝐔𝐍𝐘𝐎𝐍𝐆𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐊𝐔𝐅𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐔𝐀𝐉𝐈 𝐊𝐀𝐓𝐀𝐕𝐈

Picha
  Mahakama Kuu ya Mkoa wa Katavi imewatia hatiani na kuwahukumu watu wanne kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya mauaji ya kukusudia mtu mmoja huko katika Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi. Waliohukumiwa katika kesi hiyo ya mauaji ni Mwalemi Luyangula (23) mkazi wa Usevya, Lucia Julius (34) mkazi wa Inyonga, Kashindye Ikandago (36) mkazi wa Inyonaga na Lusoloja Machiha (28) mkazi wa Sikonge. Akisoma hukumu hiyo Mhe. Hakimu Mfawidhi Gwayi Sumaye amesema washitakiwa walitenda kosa hilo Juni 01, 2024 huko katika Kijiji cha Inyonga, Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi baada ya kumuua kwa makusudi mtu mmoja aitwaye Jilala Kanengo Nkola (48), mkazi wa Inyonga kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali (panga) sehemu mbalimbali za mwili wake akituhumiwa kuwa ni mshirikina katika kijiji hicho. Kesi hiyo namba 577/2024 ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 08, 2024 na hukumu kutolewa Mei 18, 2026 ambapo Hakimu Mfawidhi amebainisha kuwa mahakama im...

𝐑𝐂 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀 𝐀𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐀 𝐌𝐀𝐏𝐈𝐍𝐃𝐔𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎

Picha
Jarida la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga la Januari–Machi 2026 linaonesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta tofauti ikiwemo miundombinu, afya, elimu, kilimo, uwekezaji na huduma za kijamii. Katika kipindi hiki , serikali imeendelea kuboresha huduma kwa wananchi kupitia miradi ya maendeleo na usimamizi wa karibu wa shughuli za kiuchumi na kijamii. Jarida hilo pia linaonyesha jitihada za kukuza uchumi wa mkoa kwa kuongeza uwekezaji na kuboresha mazingira ya huduma za umma. Kwa ujumla , linaonesha Shinyanga ikiendelea kupiga hatua katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia utekelezaji wa mipango ya serikali. JARIDA LA MKOA WA SHINYANGA 2026 Toleo No.001 | January - March 2026 📖 SOMA FULLSCREEN ⬇ DOWNLOAD PDF

𝐖𝐀𝐒𝐈𝐎𝐉𝐔𝐋𝐈𝐊𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐌𝐂𝐇𝐎𝐌𝐀 𝐌𝐎𝐓𝐎 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐌𝐊𝐄

Picha
Jeshi la Polisi nchini Kenya limesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa shambulio la kuchomwa moto kwa mwanamke aliyesambaa mitandaoni baada ya kuchora tattoo ya Rais William Ruto pamoja na kauli za kisiasa mwilini mwake huwenda lilihusishwa na msimamo wa kisiasa. Kwa mujibu wa Polisi , mwanamke huyo alivamiwa na watu wasiojulikana katika eneo la Mwiki jijini Nairobi na kumwagiwa petroli kabla ya kuwashwa moto, tukio lililomuacha na majeraha ya moto yanayokadiriwa kufikia asilimia 70 ya mwili wake. Awali alipelekwa katika Hospitali ya Uzima Uhai kabla ya kuhamishiwa Kenyatta National Hospital kwa ajili ya matibabu maalum huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea. Kwa ujumla , Jeshi la Polisi nchini Kenya linaendelea na uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na tukio hilo huku wananchi wakitaka haki ichukuliwe dhidi ya wahusika

𝐒𝐇𝐈𝐍𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀: 𝐁𝐈𝐋𝐀 𝐀𝐉𝐀𝐋𝐈 𝐈𝐍𝐀𝐖𝐄𝐙𝐄𝐊𝐀𝐍𝐀

Picha
Na, Thadeo Gelema   Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kuzuia ajali zisizo za lazima wawapo barabarani  Picha: Bodaboda wakipewa elimu ya usalama barabarani   Akitoa elimu hiyo leo may 8, 2026 kituo Cha Polisi Wilaya ya Shinyanga Mkuu wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Shinyanga Mrakibu msaidizi wa Polisi Zainabu Mangara amewataka madereva wa pikipiki kufuata Sheria za usalama barabarani pasipo shuruti ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo ya vyombo vyao moto, kuacha kubeba abiria zaidi ya mmoja kwenye pikipiki, kukata bima ya chombo Cha moto pamoja na kuheshimu watumiaji wengine wa barabara. Picha: ASP Zainabu Mangara akizungumza na madereva wa pikipiki.   Aidha,  Mangara amewaasa kuwa mabalozi wa usalama barabarani Kwa kukemeana wao Kwa wao kuacha vitendo visivyofaa kama kuharibu bomba la mfumo wa utoaji Moshi kitu kinachopelekea utoaji wa sauti za milipuko kwenye pikipiki. Pich...

WATENDAJI TUMIENI USHAWISHI KUVUTIA WAWEKEZAJI

Picha
Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Nchemba amewataka watendaji katika taasisi na mamlaka za Serikali wawe tayari kuwawezesha wawekezaji badala ya kuwadhibiti ili wavutiwe kuwekeza zaidi na zaidi. “Nitoe wito kwa taasisi na mamlaka za Serikali, tumieni muda mwingi kuwawezesha wawekezaji badala ya kuwadhibiti. Washawishini waongeze uwekezaji badala ya kuwafanya waonekane wanaomba. Tumieni vivutio zaidi ili washawishike zaidi na zaidi,” amesema. Ametoa wito huo leo (Ijumaa, Mei 8, 2026) wakati akizungumza na wadau waliohudhuria uzinduzi wa hoteli ya Mikumi Wildlife katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, wilayani Kilosa, mkoani Morogoro. Amesema hoteli hiyo ambayo zamani ilikuwa inamilikiwa na serikali lakini ikapata janga la kuungua moto, ina historia ya miaka mingi; na ana imani na uwekezaji uliofanyika kwani umesaidia kuongeza ajira na kipato kwa wananchi. “Sina shaka uwekezaji huu utaongeza mvuto kutokana na viwango vilivyopo kwenye hoteli hii. Viwango vya hoteli hii ni vya juu sana, ninaamini vitasa...

SHINYANGA KUNUFAIKA NA KAMPENI YA SAMIA LEGAL AID

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ,Mboni Mhita akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kampeni ya Samia Legal Aid. Na Mwandishi Wetu Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuchangamkia fursa ya kupata huduma za msaada wa kisheria kupitia kampeni ya Samia Legal Aid Campaign itakayofanyika kuanzia Jumatano, Mei 5 6, 2026 mpaka Mei 20, 2026 katika halmashauri zote sita za mkoa huo. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 6,2026 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kampeni ya Samia Legal Aid mwaka 2023, imewasaidia wananchi wengi wa mkoa huo.  "Kwa awamu ya kwanza, wananchi 22,261 walikuwepo katika kampeni hiyo, ambapo migogoro 578 ilipokelewa, ikiwemo migogoro 317 iliyopatiwa utatuzi wa papo kwa papo na 261 iliyobaki kufanyiwa kazi," amesema Mhita. Mhita pia amebainisha kuwa huduma hii inatolewa bure kwa siku kumi na tano kuanzia  Mei 5 2026 mpaka Mei 20, 2026 katika  halmashauri zote za wilaya mkoa wa Shinyanga ambazo  ni Manispaa ya S...