𝐌𝐖𝐈𝐍𝐘𝐈; 𝐒𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐈𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐌𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐔𝐑𝐀𝐈𝐒

Na, Thadeo Gelema 
ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesitisha rasmi mijadala inayohusu kuongeza muda wa urais wake zaidi ya miaka 10 iliyowekwa kikatiba, akisisitiza kuwa hana nia hiyo na kwamba mjadala huo hauna tija yoyote.


Dkt. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo, Mei 23, 2026, alipofungua Jukwaa la Wenyeviti na Wakuu wa Taasisi za Umma katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, Airport, Mkoani Mkoa wa Mjini Magharibi.

​Alieleza kuwa viongozi walioapa kulinda Katiba wanapaswa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, na kubainisha kuwa kipindi kilichobaki cha uongozi wake kitalenga utekelezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo na sio mijadala isiyo na tija.

​Mashirika ya Umma Kupunguziwa Ruzuku

​Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Mwinyi ametoa onyo kali kwa mashirika ya umma yanayoendelea kutegemea ruzuku na mishahara kutoka serikalini badala ya kujiendesha kwa tija na faida.

​"Serikali haitakuwa tayari kuendelea kubeba mzigo wa mashirika ya umma yanayotegemea ruzuku... Serikali itatoa muda mfupi kwa mashirika hayo kujipanga kujiendesha kwa faida, na yatakayoshindwa, serikali haitakuwa tayari kuendelea nayo," amesisitiza Rais Mwinyi.

​Miradi ya Kimkakati na Dira ya 2050

​Sambamba na hayo, Dkt. Mwinyi amesema serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050 na kuimarisha miradi ya kimkakati ikiwemo:

  • ​Maendeleo ya Bandari
  • ​Viwanja vya Ndege
  • ​Viwanja vya Michezo
  • ​Miundombinu ya Barabara

kwa ujumla, Lengo kuu la miradi hii ni kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uchumi endelevu na wa kisasa. Alihitimisha kwa kuwataka wenyeviti na watendaji wote wa taasisi hizo kutumia vizuri fursa zilizopo nchini ili kuongeza mapato na ufanisi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀