BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI
DAR ES SALAAM: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi katika taasisi mbalimbali za umma nchini.
Na, Thadeo Gelema
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo Ijumaa, Mei 22, 2026, na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo unajumuisha viongozi wafuatao waliopangiwa
kusimamia bodi hizo muhimu:
Orodha ya Walioteuliwa na Taasisi Zao:
Ludovick James Nduhiye – Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

Dkt. Irene Charles Isaka – Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Jamhuri Joseph Ngelime – Ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
kwa ujumla, Ufanisi Katika Utendaji
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na Millard Ayo UPDATES, uteuzi huu wa viongozi unatarajiwa kuongeza kasi ya kiutendaji, uwajibikaji, pamoja na kuboresha mifumo ya usimamizi katika taasisi hizo za kimkakati kwa maendeleo ya nchi.


Maoni
Chapisha Maoni