Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2025

Habari

Picha
  HABARI PICHA: ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU CHUONI  WALIVYO JITOKEZA KWA WINGI. picha ikionesha madaktari pamoja na wanafunzi wakiwa kwenye harakiti za zoezi lauchangiaji damu. Na: Thadeo Gelema SHINYANGA, Wanafunzi na watumishi wa chuo walijitokeza kwa wingi jana kushiriki mafunzo na zoezi maalumu la uchangiaji damu lililofanyika katika presentation room chuoni hapa. Zoezi hilo lilianza saa 4:00 asubuhi, likiwa na lengo la kuwahamasisha vijana na jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu hospitalini. Mhudumu wa afya akimpima mwanafunzi  kama sehemu ya uchunguzi wa awali kabla ya zoezi Katika tukio hilo, wanafunzi waishio hostel na wale wa nje ya hostel walihudhuria kwa pamoja, wakionesha umoja na moyo wa kujitolea. Mwanafunzi akitoa damu kwa hiari, ishara ya moyo wa kujitolea miongoni mwa vijana wa chuo. Watumishi wa chuo nao walishiriki kwa hatua mbalimbali za maandalizi na uhamasishaji. Mmoja ya wanafunzi akifurahia ku...

Makala

Picha
 Je, Unataka Kuanzisha Biashara? Hii Inakuhusu Na: Thadeo Media  Kwa mujibu wa McKinsey & Company pamoja na REPOA Tanzania, maandalizi sahihi ndiyo siri ya mafanikio ya biashara mpya. Tafiti zao zinaonyesha kuwa zaidi ya 70% ya biashara zinazodumu ni zile zilizotumia muda kufanya utafiti kabla ya kuanza. 1. Utafiti wa Soko Makampuni haya ya utafiti yanaeleza kuwa hatua ya kwanza ni kuelewa mahitaji ya wateja. Bila kujua uhitaji, hata mtaji mkubwa hauwezi kuokoa biashara. 2. Mtaji na Bajeti Ripoti za McKinsey zinaonyesha kuwa biashara nyingi hufa mapema kwa sababu ya kutopanga mtaji wa uendeshaji. Jua gharama za mwanzo, gharama za kila mwezi, na fedha za dharura. 3. Kuelewa Ushindani Kwa mujibu wa REPOA, biashara nyingi hushindwa kwa kutopima washindani. Jiulize: Nani tayari yupo sokoni? Wanafanya nini vizuri? Utofauti wako ni upi? 4. Eneo au Uwepo Mtandaoni Utafiti unaonyesha kuwa eneo sahihi linaongeza wateja kwa kiwango kikubwa. Kwa biashara za mtandaoni, uimara wa kuras...

Makala

Picha
  Kwa Nini Vitendo Vidogo vya Upendo Vinajenga Uhusiano Mkubwa? Na Thadeo Media  Kwa Mujibu wa Dkt. Kory Floyd** Katika dunia ya leo yenye presha nyingi, wengi wamekuwa wakiamini kwamba ili uhusiano uendelee kuimarika, unahitaji maneno makubwa au zawadi za gharama. Lakini ukweli hauko hivyo. Tafiti nyingi za mawasiliano ya kimapenzi zimeonyesha kuwa mambo madogo ya kila siku ndiyo yanayounda msingi imara wa mahusiano yenye upendo na kuaminiana. Kwa mujibu wa Dkt. Kory Floyd, mtaalamu mashuhuri wa mawasiliano kutoka University of Arizona, vitendo vidogo kama kutuma meseji ya “umeamkaje?”, “umefikaje?”, au hata kutuma emoji ya moyo, vina nguvu ya kuongeza ukaribu wa kihisia kuliko maneno makubwa yanayotolewa mara chache. Dkt. Floyd anajulikana kwa kazi yake ndani ya Affection Exchange Theory, ambayo inaeleza jinsi mawasiliano madogo ya upendo yanavyoathiri hisia za mtu, afya ya uhusiano, na hata ustawi wa mwili. Anaamini kuwa simultaneously, tabia rahisi kama kuonyesha kujali ma...

Makala

Picha
 Kwa Nini Vijana Wengi Tanzania Wanachagua Biashara Ndogo Badala ya Kusubiri Ajira? Na: Thadeo Media  Katika muktadha wa uchumiwa sasa, Tanzania imekuwa ikishuhudia mabadiliko makubwa katika maisha ya vijana. Wakati zamani wengi walitegemea ajira rasmi za ofisini au za sekta ya umma, kizazi cha sasa kimeanza kuangalia njia mbadala za kujitengenezea kipato. Biashara ndogo ndogo imekuwa chaguo maarufu, hasa miongoni mwa vijana wa umri wa miaka 18–35. Makala hii inachambua sababu, takwimu, na mwelekeo huu kwa mujibu wa tafiti la Afrobarometer Round 10 (2025) na mtazamo wa kitaaluma wa uandishi wa habari. 1. Ukosefu wa ajira rasmi ni changamoto kubwa Kwa mujibu wa Afrobarometer (2025), 26% ya vijana wa Tanzania (18–35) hawana ajira rasmi. Hali hii inaonyesha kwamba kijana mmoja kati ya wanne hawezi kupata nafasi ya ajira katika sekta ya umma au binafsi. Kwa vijana hawa, biashara ndogo ndogo ni njia ya haraka ya kupata kipato, badala ya kukaa bila shughuli au kusubiri nafasi ambazo...

Habari

Picha
St.Joseph’s College Shinyanga Watembelea Watoto Wenye Mahitaji Maalumu Na Thadeo Media  Leo Tarehe 22 Novemba 2025, kuanzia mapema asubuhi, wanafunzi pamoja na wakufudhi wa St Joseph’s College Shinyanga walifanya ziara ya kijamii katika kituo cha Burugalila, kilichopo Kizumbi, Shinyanga Mjini, kwa ajili ya kuwafariji watoto wenye mahitaji maalum. Picha wanafunzi, wakufunzi na watoto wenye uhitaji maalumu Burugalila  Katika ziara hiyo, wanafunzi pamoja na wakufudhi walitoa misaada mbalimbali ikiwemo vyakula, sabuni, na vifaa vingine muhimu. Aidha, walipata nafasi ya kuzungumza na watoto hao ili kuwapa faraja na kuwafanya wajisikie kupendwa na kuthaminiwa. Picha wanafunzi wenye mahitaji maalumu Burugalila wakiwa na wakufunzi, wanafunzi na pamoja na walezi Wakufunzi walisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwajengea wanafunzi moyo wa kujitolea, uwajibikaji na kujifunza umuhimu wa kushiriki katika shughuli za kijamii. Picha Burugalila  Uongozi wa kituo cha Burugalila uliwashukur...

Makala

Picha
  KWANINI VIJANA WA LEO WANACHUKIA KUOLEWA NA KUOA MAPEMA TOFAUTI NA ZAMANI? Na: Thadeo Media Katika jamii ya sasa, watu wengi wameanza kuona kuolewa mapema kama jambo lisilo tena kipaumbele kwa vijana, tofauti na miaka ya nyuma ambapo ndoa ya mapema ilikuwa sehemu ya maisha ya kawaida.  Makala hii inaangalia kwa mujibu wa hali ya sasa na inalinganisha mabadiliko ya kihistoria yaliyobadilisha mtazamo wa vijana kuhusu ndoa. 1. ZAMANI: NDOA YA MAPEMA ILIKUWA NI DESTURI | LEO: NDOTO NA ELIMU ZIMEKUWA KIPAUMBELE Kihistoria (Kabla ya 1980s) Katika jamii nyingi za Tanzania kama Wasukuma, Wapare, Waha, Wanyamwezi, na Wamagharibi mwa nchi: Kuolewa mapema kuliheshimika Kulionekana kama hatua ya utu uzima Familia ziliona ni njia ya kuimarisha ukoo Kwa Mujibu wa Jamii ya Sasa (2000–2025) Vijana leo wanataka: Elimu Kazi yenye uhakika Kujijenga kwanza kabla ya majukumu Kwa hiyo kuolewa mapema “hakusomeki” katika malengo yao ya maisha. 2. ZAMANI: UCHUMI ULIKUWA ATHARI NDOGO | LEO: GARMA ZA ...