Habari

 HABARI PICHA: ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU CHUONI  WALIVYO JITOKEZA KWA WINGI.

picha ikionesha madaktari pamoja na wanafunzi wakiwa kwenye harakiti za zoezi lauchangiaji damu.

Na: Thadeo Gelema

SHINYANGA, Wanafunzi na watumishi wa chuo walijitokeza kwa wingi jana kushiriki mafunzo na zoezi maalumu la uchangiaji damu lililofanyika katika presentation room chuoni hapa.

Zoezi hilo lilianza saa 4:00 asubuhi, likiwa na lengo la kuwahamasisha vijana na jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu hospitalini.

Mhudumu wa afya akimpima mwanafunzi  kama sehemu ya uchunguzi wa awali kabla ya zoezi
Katika tukio hilo, wanafunzi waishio hostel na wale wa nje ya hostel walihudhuria kwa pamoja, wakionesha umoja na moyo wa kujitolea.

Mwanafunzi akitoa damu kwa hiari, ishara ya moyo wa kujitolea miongoni mwa vijana wa chuo.

Watumishi wa chuo nao walishiriki kwa hatua mbalimbali za maandalizi na uhamasishaji.

Mmoja ya wanafunzi akifurahia kuhusu umuhimu wa uchangiaji damu

Wanafunzi wakisajiliwa kabla ya kuanza zoezi la uchangiaji damu ndani ya ukumbi wa presentation room.
Tukio hili limeacha ujumbe muhimu kwa vijana kuhusu nafasi yao katika kuokoa maisha kupitia uchangiaji damu.


Matangazo 





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀