Habari
St.Joseph’s College Shinyanga Watembelea Watoto Wenye Mahitaji Maalumu
Na Thadeo Media
Leo Tarehe 22 Novemba 2025, kuanzia mapema asubuhi, wanafunzi pamoja na wakufudhi wa St Joseph’s College Shinyanga walifanya ziara ya kijamii katika kituo cha Burugalila, kilichopo Kizumbi, Shinyanga Mjini, kwa ajili ya kuwafariji watoto wenye mahitaji maalum.
| Picha wanafunzi, wakufunzi na watoto wenye uhitaji maalumu Burugalila |
Katika ziara hiyo, wanafunzi pamoja na wakufudhi walitoa misaada mbalimbali ikiwemo vyakula, sabuni, na vifaa vingine muhimu. Aidha, walipata nafasi ya kuzungumza na watoto hao ili kuwapa faraja na kuwafanya wajisikie kupendwa na kuthaminiwa.
| Picha wanafunzi wenye mahitaji maalumu Burugalila wakiwa na wakufunzi, wanafunzi na pamoja na walezi |
Wakufunzi walisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwajengea wanafunzi moyo wa kujitolea, uwajibikaji na kujifunza umuhimu wa kushiriki katika shughuli za kijamii.
| Picha Burugalila |
Uongozi wa kituo cha Burugalila uliwashukuru wanafunzi na walimu kwa upendo na msaada walioutoa, wakisema umeleta matumaini na tabasamu kwa watoto hao.
| Picha Burugalila Ziara hii imeendelea kuwa sehemu ya mafunzo ya kukuza utu, mshikamano na huruma miongoni mwa wanafunzi na wakufudhi wa St Joseph’s College Shinyanga. Matangazo |
Hongera sana kwa kufanya hivo,hata Mungu anapendezwa nacho,chuo cha st.joseph mbarikiwe Sanaππ»ππ»
JibuFuta