𝐇𝐔𝐊𝐔𝐌𝐔: 𝐌𝐈𝐀𝐊𝐀 80 𝐉𝐄𝐋𝐀,𝐕𝐈𝐁𝐎𝐊𝐎 6 𝐍𝐀 𝐅𝐈𝐃𝐈𝐀 𝐌𝐈𝐋𝐈𝐎𝐍𝐈 26
Na, Mwandishi wetu
KATAVI: Mahakama ya Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi imemtia hatiani na kumhukumu kifungo cha jumla ya miaka 80 jela Bw. Jofrey Musa Masanja (27), baada ya kupatikana na hatia ya makosa sita (06) ya unyang'anyi wa kutumia silaha na kujeruhi.
Mbali na kifungo hicho cha miaka 80 jela, Mahakama pia imempa adhabu ya kuchapwa viboko sita (06), kulipa fidia ya jumla ya shilingi milioni 10 (10,000,000 TZS) kwa majeruhi wote, pamoja na kurudisha kiasi cha shilingi milioni 16 (16,000,000 TZS) kilichoibiwa.
Ukatili Aliotenda kwa Nyakati Tofauti
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Sylivester Makombe, ameeleza kuwa mshitakiwa alitenda makosa hayo ya kikatili katika Kijiji cha Vikonge wilayani Tanganyika kwa nyakati tatu tofauti mnamo Novemba 2024:
Novemba 19, 2024: Alimvamia na kumfunga kamba mwili mzima mwananchi John Burunda, kisha kumshambulia na kumuibia kiasi cha shilingi 60,000.
Novemba 22 na Novemba 26, 2024: Akitumia silaha yenye ncha kali (kisu) na fimbo, alimjeruhi vibaya tena John Burunda na kumuibia kiasi cha shilingi 16,160. Katika matukio hayo, mtuhumiwa pia aliwajeruhi vibaya sehemu mbalimbali za miili yao wananchi wengine watatu ambao ni Misalaba Kabalo, Mushilu Musa, na Pascal Macheyeki.
Safari ya Kesi Hadi Hukumu
Kesi hiyo yenye namba 11478/2025 ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Machi 3, 2025. Baada ya mchakato wa kisheria kuchukua zaidi ya mwaka mmoja, hukumu imetolewa rasmi Mei 12, 2026.
Hakimu Makombe amesisitiza kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo shaka yoyote na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri kupitia mashahidi 10, ambao ulikamilika na kutosha kumtia hatiani mshitakiwa huyo kwa makosa yote sita yaliyokuwa yanamkabili.
👉kwa ujumla, Kupata taarifa za kina za kisheria na matukio mengine ya mahakamani, endelea. Kutembelea : thadeomedia5.blogspot.com

Maoni
Chapisha Maoni