𝐌𝐀𝐌𝐀 𝐊𝐔𝐔𝐏𝐈𝐆𝐀 𝐌𝐖𝐈𝐍𝐆𝐈, 𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐍𝐈𝐒𝐇𝐀𝐓𝐈 𝐘𝐀 𝐍𝐘𝐔𝐊𝐋𝐈𝐀 𝐀𝐅𝐑𝐈𝐊𝐀

Na, Thadeo Gelema 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali ambapo atashiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA), Kigali nchini Rwanda Mei 19, 2026.

Mkutano huo wa Kimataifa unawakutanisha pia wataalamu wa nishati, wawekezaji na mashirika ya kimataifa, ambapo utajadili matumizi ya nishati ya nyuklia kwa maendeleo ya Bara la Afrika. Mkutano huo pia unalenga kujadili namna bora ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme Afrika, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kusaidia maendeleo ya viwanda, kukuza ubunifu wa teknolojia za nishati ya nyuklia pamoja na kuvutia wawekezaji katika miradi ya nishati.

Kwa ujumla, Mkutano huo unatajwa kuwa hatua muhimu kwa Afrika katika kutafuta suluhisho la nishati safi, maendeleo ya teknolojia na kuongeza uwekezaji utakaosaidia kukuza uchumi na viwanda barani humo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀