𝐖𝐀𝐍𝐍𝐄 𝐊𝐔𝐍𝐘𝐎𝐍𝐆𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐈 𝐊𝐔𝐅𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐔𝐀𝐉𝐈 𝐊𝐀𝐓𝐀𝐕𝐈
![]() |
Mahakama Kuu ya Mkoa wa Katavi imewatia hatiani na kuwahukumu watu wanne kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya mauaji ya kukusudia mtu mmoja huko katika Kijiji cha Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi.
Waliohukumiwa katika kesi hiyo ya mauaji ni Mwalemi Luyangula (23) mkazi wa Usevya, Lucia Julius (34) mkazi wa Inyonga, Kashindye Ikandago (36) mkazi wa Inyonaga na Lusoloja Machiha (28) mkazi wa Sikonge.
Akisoma hukumu hiyo Mhe. Hakimu Mfawidhi Gwayi Sumaye amesema washitakiwa walitenda kosa hilo Juni 01, 2024 huko katika Kijiji cha Inyonga, Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi baada ya kumuua kwa makusudi mtu mmoja aitwaye Jilala Kanengo Nkola (48), mkazi wa Inyonga kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali (panga) sehemu mbalimbali za mwili wake akituhumiwa kuwa ni mshirikina katika kijiji hicho.
Kesi hiyo namba 577/2024 ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 08, 2024 na hukumu kutolewa Mei 18, 2026 ambapo Hakimu Mfawidhi amebainisha kuwa mahakama imejiridhisha pasiposhaka na ushahidi uliotolewa na mashaidi 19 kutoka upande wa Jamhuri na umetosha kuwatia hatiani watuhumiwa hao.
Kwa ujumla, Mahakama Kuu ya Katavi imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu wanne kwa mauaji ya kukusudia, hatua inayothibitisha msimamo mkali dhidi ya uhalifu na kulinda uhai wa binadamu.

Maoni
Chapisha Maoni