𝐊𝐈𝐊𝐀𝐀𝐍𝐆𝐎𝐍𝐈 𝐊𝐔𝐋𝐀𝐖𝐈𝐓𝐈 𝐌𝐓𝐎𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐌𝐈𝐀𝐊𝐀 6

 Na,Thadeo Gelema 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Kesi Juma Ibrahim, Miaka 22, Mkulima na mkazi wa Kifuleta, Chalinze kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka 6 (Jina linahifadhiwa).

Mnamo Mei 17, 2026 majira ya saa 7:00 mchana huko katika Kijiji cha Kifuleta, Kata ya Kimange, Chalinze mtuhumiwa alimlaghai mtoto huyo ambaye ni jirani yake na kumuingiza chumbani kwake kisha kumfanyia kitendo hicho.

Baada ya wazazi kugundua kuwa mtoto amefanyiwa kitendo hicho waliripoti kituo cha Polisi Mbwewe ambapo jitihada zilifanyika na mtuhumiwa huyo kukamatwa.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea na upelelezi na mara utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.

Kwa ujumla, Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea na upelelezi wa tukio hilo, huku likisisitiza kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀