𝐀𝐉𝐀𝐋𝐈 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀: 𝐌𝐌𝐎𝐉𝐀 𝐀𝐅𝐀𝐑𝐈𝐊𝐈, 𝐖𝐀𝐀𝐍𝐃𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐒𝐀𝐁𝐀 𝐌𝐀𝐉𝐄𝐑𝐔𝐇𝐈


Shinyanga

Mpiga picha wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Boaz Martine amefariki dunia huku waandishi wa habari Frank Mshana wa ITV/Radio One na Johnson James wakiwa miongoni mwa watu saba waliojeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea Mei 19, 2026 katika Kata ya Samuye, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba T.210 EDB na Toyota Land Cruiser Hardtop lenye namba DFPA 8920 mali ya shirika la KOICA, lililokuwa limebeba waandishi wa habari pamoja na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 20, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Janeth Magomi amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Toyota Harrier aliyekuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari, hali iliyosababisha kugongana na Land Cruiser hiyo na kutumbukia mtaroni.

Mbali na Frank Mshana na Johnson James afisa habari ofisi ya mkuu wa Mkoa, majeruhi wengine ni Koplo Swahiba Msangi, Neema Madono (36), Rehema Edson (45), Shadia Omari (32) pamoja na dereva wa Land Cruiser Laurence Peter (34). 

Majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamanda Magomi ametoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litachukua hatua za kisheria dhidi ya madereva watakaobainika kusababisha ajali kwa uzembe.

Kwa ujumla, Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limetoa wito kwa madereva kuzingatia sheria na tahadhari barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kusababisha vifo na majeruhi, huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea na hatua za kisheria zikitarajiwa kuchukuliwa dhidi ya waliohusika.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀