𝐖𝐀𝐒𝐈𝐎𝐉𝐔𝐋𝐈𝐊𝐀𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐌𝐂𝐇𝐎𝐌𝐀 𝐌𝐎𝐓𝐎 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐌𝐊𝐄

Jeshi la Polisi nchini Kenya limesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa shambulio la kuchomwa moto kwa mwanamke aliyesambaa mitandaoni baada ya kuchora tattoo ya Rais William Ruto pamoja na kauli za kisiasa mwilini mwake huwenda lilihusishwa na msimamo wa kisiasa.

Kwa mujibu wa Polisi, mwanamke huyo alivamiwa na watu wasiojulikana katika eneo la Mwiki jijini Nairobi na kumwagiwa petroli kabla ya kuwashwa moto, tukio lililomuacha na majeraha ya moto yanayokadiriwa kufikia asilimia 70 ya mwili wake.

Awali alipelekwa katika Hospitali ya Uzima Uhai kabla ya kuhamishiwa Kenyatta National Hospital kwa ajili ya matibabu maalum huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Kwa ujumla, Jeshi la Polisi nchini Kenya linaendelea na uchunguzi wa kuwabaini waliohusika na tukio hilo huku wananchi wakitaka haki ichukuliwe dhidi ya wahusika


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀