𝐒𝐇𝐈𝐍𝐘𝐀𝐍𝐆𝐀: 𝐁𝐈𝐋𝐀 𝐀𝐉𝐀𝐋𝐈 𝐈𝐍𝐀𝐖𝐄𝐙𝐄𝐊𝐀𝐍𝐀
Na, Thadeo Gelema
Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kuzuia ajali zisizo za lazima wawapo barabarani
![]() |
| Picha: Bodaboda wakipewa elimu ya usalama barabarani |
Akitoa elimu hiyo leo may 8, 2026 kituo Cha Polisi Wilaya ya Shinyanga Mkuu wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Shinyanga Mrakibu msaidizi wa Polisi Zainabu Mangara amewataka madereva wa pikipiki kufuata Sheria za usalama barabarani pasipo shuruti ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo ya vyombo vyao moto, kuacha kubeba abiria zaidi ya mmoja kwenye pikipiki, kukata bima ya chombo Cha moto pamoja na kuheshimu watumiaji wengine wa barabara.
![]() |
| Picha: ASP Zainabu Mangara akizungumza na madereva wa pikipiki. |
Aidha, Mangara amewaasa kuwa mabalozi wa usalama barabarani Kwa kukemeana wao Kwa wao kuacha vitendo visivyofaa kama kuharibu bomba la mfumo wa utoaji Moshi kitu kinachopelekea utoaji wa sauti za milipuko kwenye pikipiki.
![]() |
| Picha: Madereva wakihimizwa kufuata sheria za barabarani |
Kwa upande wao Maafisa usafirishaji hao wamelishukuru Jeshi la Polisi Kwa kuwapatia elimu hiyo na kukiri kuwa mabalozi wazuri wa kufuata Sheria ya usalama barabarani ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kupelekea vifo, majeruhi pamoja na uharibifu wa vyombo vya moto.
![]() |
| Picha: mbalimbali Elimu ya usalama ikitolewa kupunguza ajali Shinyanga. |


Kwa ujumla, elimu hiyo inalenga kuwajengea madereva wa bodaboda uelewa wa kufuata sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali, kulinda maisha ya wananchi na kuhakikisha usalama wa watumiaji wote wa barabara.





Maoni
Chapisha Maoni