Maisha ya chuoni
GARAGE FC vs ST. JOSEPH’S COLLEGE FC: IJUMAA HII, Baada ya Mitihani, Sasa Ni Muda wa Burudani – Ijumaa Hii Laini Polisi
Shinyanga, Julai 31, 2025
Na: Thadeo Media
Baada ya kumaliza mitihani ya mwisho kwa mafanikio makubwa, wanafunzi wa St. Joseph’s College of Shinyanga (STJOSO) sasa wanajiandaa kwa burudani kabambe kupitia tukio maalum la michezo litakalowakutanisha na Garage FC kwenye mechi ya kirafiki yenye mvuto wa kipekee.
Mechi hiyo itachezwa Ijumaa hii, Agosti 1, 2025, kuanzia saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Laini Polisi – Shinyanga. Ni fursa adimu kwa wanafunzi, wakufunzi na wadau wa elimu kuungana pamoja kusherehekea mafanikio ya kitaaluma kupitia ushindani wa kiwanjani.
“Mchezo huu si tu burudani, bali pia ni njia ya kujenga mshikamano wa kijamii na kupunguza msongo wa mawazo baada ya mitihani,” amesema Waziri wa Habari wa STJOSO.
👉 Kila Mtu Anakaribishwa:
Wanafunzi wa chuo, walimu, wahitimu, marafiki na wadau wa michezo – mnaombwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hili la kusisimua. Usikose fursa hii ya kufunga wiki kwa kelele za furaha na hamasa.
Burudani Haishi Uwanjani – Bash Kubwa SPC Club!
Mara baada ya mechi kumalizika, kutakuwa na Bash ya usiku ya nguvu itakayofanyika SPC Club, kwa ajili ya kuendeleza furaha na kusherehekea pamoja. Taarifa kamili kuhusu muda wa bash hiyo itatolewa mapema kabla ya siku ya tukio.
Muhtasari wa Tukio:
Tukio: Mechi ya kirafiki – Garage FC vs STJOSO FC
Tarehe: Ijumaa, Agosti, 2025
Muda: Saa 10:00 jioni
Mahali: Uwanja wa Laini Polisi – Shinyanga
Burudani: Bash ya usiku @ SPC Club (Muda utatangazwa)
Maoni
Chapisha Maoni