Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Maisha ya chuoni

𝐂𝐇𝐄𝐓𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐙𝐈𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐁𝐀𝐑𝐈 𝐒𝐓𝐉𝐎𝐒𝐎 2𝐎25/26

Picha
Na, Thadeo Gelema  Katika hafla ya uapisho iliyofanyika Jumatatu, Aprili 13, 2026 chuoni hapo, viongozi mbalimbali walitunukiwa vyeti vya heshima kutokana na mchango wao katika uongozi na maendeleo ya wanafunzi. Miongoni mwa waliotunukiwa heshima hiyo ni Thadeo Gelema, aliyekuwa Waziri wa Habari STJOSO 2025/26, akitambuliwa kwa juhudi zake katika kukuza sekta ya habari ndani ya chuo hicho. Tuzo hiyo imeibua mjadala miongoni mwa wanafunzi na wadau wa habari, wakijiuliza iwapo hii ni ishara ya mwanzo mpya wa kuimarika kwa Thadeo haswa katika masuala ya habari 📲 Endelea kufuatilia na soma zaidi 👇👇 @thadeomedia5.blogspot.com

𝐒𝐇𝐀𝐑𝐎𝐍 𝐀𝐀𝐏𝐈𝐒𝐇𝐖𝐀 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐌𝐏𝐘𝐀 𝐒𝐓𝐉𝐎𝐒𝐎 2026/27, 𝐕𝐈𝐂𝐄𝐍𝐓 𝐀𝐓𝐎𝐀 𝐔𝐒𝐇𝐀𝐔𝐑𝐈 𝐌𝐙𝐈𝐓𝐎

Picha
  Na Thadeo Gelema, Shinyanga Leo Aprili 13, 2026 Rais mpya wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) 2026/2027, Sharon Callist Mathias,   ameapishwa rasmi kushika wadhifa huo, akiahidi kuanza kazi mara moja kwa kushughulikia changamoto zinazowakabili wanafunzi, ikiwemo suala la bima ya afya ambalo amelipa kipaumbele cha juu. Hafla ya kuapishwa iliyofanyika chuoni hapo imehudhuriwa na viongozi wa chuo, wanafunzi pamoja na wageni mbalimbali, huku ikitawaliwa na matumaini mapya ya uongozi. Akizungumza baada ya kula kiapo, Sharon alisema kuwa uongozi wake utaanza kwa kugusa mahitaji ya msingi ya wanafunzi. “ Kipaumbele changu cha kwanza ni kushughulikia changamoto ya bima ya afya kwa wanafunzi, pamoja na kuboresha upatikanaji wa vifaa vya makatibu na vifaa vya uandishi wa habari ,” alisema Shaloni. Aidha , alisisitiza kuwa ataimarisha mahusiano kati ya wanafunzi, walimu, serikali ya chuo pamoja na taasisi binafsi ili kujenga mazingira bora ya kujifunzia na kushirikiana. Kwa upande ...

𝗨𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗨𝗗𝗜𝗢: 𝗦𝗛𝗔𝗥𝗢𝗡 𝗔𝗩𝗨𝗡𝗝𝗔 𝗨𝗞𝗨𝗧𝗔 𝗦𝗧𝗝𝗢𝗦𝗢

Picha
  📅 10 Aprili 2026 Shinyanga – Hatimaye pazia limefungwa katika uchaguzi wa marudio wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) 2026/2027, huku Sharon Callist Mathias akiandika historia kwa kuibuka mshindi na kuwa Rais mpya wa wanafunzi. Uchaguzi huo uliokuwa umejaa presha, mvutano na matarajio makubwa, umegeuka kuwa gumzo kubwa chuoni hapo baada ya kuleta matokeo tofauti kabisa na uchaguzi wa awali.   MATOKEO RASMI YA MARUDIO Sharon (Shaloni) — kura 23 Vicent — kura 11 Moris Daudi — kura 8 Maduhu — kura 5 Sitta — kura 2  Jumla ya kura: 49  Hakuna kura iliyoharibika   ILIVYOKUWA MWANZO Katika uchaguzi wa kwanza, hali ilikuwa tofauti kabisa ambapo Maduhu aliongoza kwa kura 43, akifuatiwa na Sharon aliyepata kura 21. Hata hivyo, malalamiko juu ya mwenendo wa uchaguzi yalizua sintofahamu na kusababisha kurudiwa kwa uchaguzi.   MABADILIKO MAKUBWA Uchaguzi wa marudio umeonyesha mabadiliko ya wazi ya maamuzi ya wapiga kura, ambapo Shaloni ameweza kupindua upepo na kuibu...

𝗨𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗭𝗜 𝗪𝗔𝗥𝗨𝗗𝗜𝗪𝗔 𝗦𝗧𝗝𝗢𝗦𝗢: 𝗝𝗘, 𝗛𝗜𝗜 𝗡𝗗𝗜𝗢 𝗙𝗨𝗥𝗦𝗔 𝗬𝗔 𝗛𝗔𝗞𝗜 𝗔𝗨?

Picha
  Na, Thadeo Gelema  📅 08 April 2026 | ⏰ Saa 15:20 Alasiri  Shinyanga – Zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa marudio wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) limehitimishwa rasmi, lakini hadi sasa hali ya sintofahamu imeendelea kutawala baada ya matokeo kuchelewa kutangazwa. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo , zoezi la kupiga kura lilikamilika majira ya saa sita, huku kura zikihifadhiwa ndani ya chumba cha Dean of student , zikisubiri hatua zinazofuata katika mchakato wa kuhesabu na kutangaza matokeo. Hadi sasa , baadhi ya wagombea pamoja na wafuasi wao bado wapo eneo la tukio wakisubiri, huku wakitarajia uwepo wa Mkurugenzi wa chuo ili kuendelea na hatua inayofuata. Wakati huo huo, baadhi ya wanafunzi wameanza kuondoka kutokana na kuchelewa kwa mchakato huo. Hali hii imeendelea kuibua maswali miongoni mwa wanafunzi kuhusu uwazi na ufanisi wa usimamizi wa uchaguzi huo wa marudio, ambao tayari umebeba matarajio makubwa ya kurejesha imani ya wanafunzi. Kwa ujumla , Wakati mac...

𝗦𝗧𝗝𝗢𝗦𝗢: 𝗨𝗖𝗛𝗔𝗚𝗨𝗭𝗜 𝗪𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗨𝗗𝗜𝗢 , 𝗣𝗥𝗘𝗦𝗛𝗔 𝗠𝗔𝗥𝗔 𝗠𝗕𝗜𝗟𝗜!

Picha
  Na, Thadeo Gelema Shinyanga – Baada ya mvutano mkubwa, malalamiko na sintofahamu iliyotawala uchaguzi uliopita, uongozi wa Chuo cha Mt. Joseph umetangaza rasmi kurudiwa kwa uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) , hatua inayokuja wakati hali ya kisiasa chuoni ikiwa bado haijatulia. Kurudiwa kwa uchaguzi huu kumekuja kufuatia presha ya malalamiko yaliyoibuliwa na baadhi ya wagombea pamoja na wafuasi wao, waliodai kuwepo kwa mapungufu katika mchakato uliopita. Hatua hiyo sasa imegeuza uchaguzi huu kuwa zaidi ya zoezi la kawaida – bali ni mtihani wa uwazi na haki. Wagombea Tajwa, Presha Yaongezeka Katika uchaguzi huo wa marudio, Mwl. Moris Daudi ni miongoni mwa wagombea wanaotarajiwa kurejea tena uwanjani, akijiandaa kuwania nafasi hiyo kwa mara nyingine huku akibeba matumaini mapya kutoka kwa wafuasi wake. Miongoni mwa wagombea wanaotarajiwa kushiriki tena ni pamoja na Mh. Vicent Chacha , kiongozi mwenye uzoefu na msimamo thabiti, pamoja na Sitta Matias, anayesifika kwa nidha...

𝐇𝐀𝐈𝐉𝐀𝐖𝐀𝐇𝐈 𝐊𝐔𝐓𝐎𝐊𝐄𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐖𝐀𝐍𝐙𝐀!

Picha
𝘕𝘢, 𝘛𝘩𝘢𝘥𝘦𝘰 𝘔𝘦𝘥𝘪𝘢   ˢʰⁱⁿʸᵃⁿᵍᵃ – ᵘᶜʰᵃᵍᵘᶻⁱ ʷᵃ ˢᵉʳⁱᵏᵃˡⁱ ʸᵃ ʷᵃⁿᵃᶠᵘⁿᶻⁱ (ˢᵗʲᵒˢᵒ) 2026/2027 ᵘᵐᵉ ᵏᵘʷᵃ ᵐⁱᵒⁿᵍᵒⁿⁱ ᵐʷᵃ ᶜʰᵃᵍᵘᶻⁱ ᶻᵉⁿʸᵉ ᵐᵛᵘᵗᵃⁿᵒ ᵐᵏᵘᵇʷᵃ ᵏᵘʷᵃʰⁱ ᵏᵘˢʰᵘʰᵘᵈⁱʷᵃ ᶜʰᵘᵒⁿⁱ ʰᵃᵖᵒ, ʰᵃˡⁱ ᵃᵐᵇᵃʸᵒ ʰᵃⁱʲᵃʷᵃʰⁱ ᵏᵘʲⁱᵗᵒᵏᵉᶻᵃ ᵏʷᵃ ᵏⁱʷᵃⁿᵍᵒ ʰⁱᵏⁱ ᵏⁱʰⁱˢᵗᵒʳⁱᵃ. ᵗᵃᵃʳⁱᶠᵃ ᶻⁱⁿᵃᶻᵒᵉⁿᵈᵉˡᵉᵃ ᵏᵘˢᵃᵐᵇᵃᵃ ᶜʰⁱⁿⁱ ᶜʰⁱⁿⁱ ᶻⁱⁿᵃᵉˡᵉᶻᵃ ᵏᵘʷᵃ ᵇᵃᵃᵈʰⁱ ʸᵃ ʷᵃᵍᵒᵐᵇᵉᵃ ᵗᵃʸᵃʳⁱ ʷᵃᵐᵉᵃⁿᶻᵃ ᵏᵘʷᵃˢⁱˡⁱˢʰᵃ ᵐᵃˡᵃˡᵃᵐⁱᵏᵒ ʸᵃᵒ ᵏʷᵃ ᵗᵘᵐᵉ ʸᵃ ᵘᶜʰᵃᵍᵘᶻⁱ ᵏʷᵃ ⁿʲⁱᵃ ʸᵃ ᵇᵃʳᵘᵃ ʳᵃˢᵐⁱ, ʷᵃᵏⁱᵖⁱⁿᵍᵃ ᵐʷᵉⁿᵉⁿᵈᵒ ᵐᶻⁱᵐᵃ ʷᵃ ᵘᶜʰᵃᵍᵘᶻⁱ ʰᵘᵒ ʰᵃᵗᵘᵃ ʰⁱʸᵒ ⁱᵐᵉᵏᵘʲᵃ ᵏᵘᶠᵘᵃᵗⁱᵃ ᵐᵃᵈᵃⁱ ᵐᵇᵃˡⁱᵐᵇᵃˡⁱ ʸᵃˡⁱʸᵒⁱᵇᵘᵏᵃ ᵇᵃᵃᵈᵃ ʸᵃ ᵐᵃᵗᵒᵏᵉᵒ ᵏᵘᵗᵃⁿᵍᵃᶻʷᵃ, ⁱᵏⁱʷᵉᵐᵒ ʰᵒʲᵃ ᵏᵘʰᵘˢᵘ ᵘˢⁱᵐᵃᵐⁱᶻⁱ ʷᵃ ᵏᵘʳᵃ ⁿᵃ ᵘʰᵃˡᵃˡⁱ ʷᵃ ᵐᶜʰᵃᵏᵃᵗᵒ ᵐᶻⁱᵐᵃ. ʰᵃᵗᵃ ʰⁱᵛʸᵒ, ʰᵃᵈⁱ ᵏᵘᶠⁱᵏⁱᵃ ˢᵃˢᵃ, ʰᵃᵏᵘⁿᵃ ᵗᵃᵃʳⁱᶠᵃ ʳᵃˢᵐⁱ ⁱˡⁱʸᵒᵗᵒˡᵉʷᵃ ⁿᵃ ᵗᵘᵐᵉ ʸᵃ ᵘᶜʰᵃᵍᵘᶻⁱ ᵏᵘʰᵘˢᵘ ᵏᵘᵖᵒᵏᵉᵃ ᵃᵘ ᵏᵘˢʰᵘᵍʰᵘˡⁱᵏⁱᵃ ᵐᵃˡᵃˡᵃᵐⁱᵏᵒ ʰᵃʸᵒ. ʷᵃⁿᵃᶠᵘⁿᶻⁱ ʷᵃᵐᵉᵒⁿᵉᵏᵃⁿᵃ ᵏᵘᵍᵃʷᵃⁿʸⁱᵏᵃ, ᵃᵐᵇᵃᵖᵒ ᵇᵃᵃᵈʰⁱ ʷᵃⁿᵃᵗᵉᵗᵉᵃ ᵐᵃᵗᵒᵏᵉᵒ ʸᵃˡⁱʸᵒᵗᵃⁿᵍᵃᶻʷᵃ ʰᵘᵏᵘ ʷᵉⁿᵍⁱⁿᵉ ʷᵃᵏⁱˢⁱˢⁱᵗⁱᶻᵃ ᵏᵘʷᵃ ⁿⁱ ˡᵃᶻⁱᵐᵃ ʰᵃᵏⁱ ⁱᵗᵉⁿᵈᵉᵏᵉ ᵏᵃᵇˡᵃ ʸᵃ ᵏᵘᵏᵘᵇᵃˡⁱᵏᵃ ᵏʷᵃ ᵐᵃᵗᵒᵏᵉᵒ ʰᵃʸᵒ. Kwa ujumla  ʷᵃᵏᵃᵗⁱ ᵐᵃᶜʰᵒ ʸᵃᵏⁱᵉˡᵉᵏᵉᶻʷᵃ ᵏʷᵃ ᵗᵘᵐᵉ ʸᵃ ᵘᶜʰᵃᵍᵘᶻⁱ, ʷᵉⁿᵍⁱ ʷᵃⁿᵃˢᵘᵇⁱʳⁱ ᵏᵘᵒ...

MATOKEO YA UCHAGUZI STJOSO 2026/2027 YAZUA MJADALA

Picha
Na Mwandishi wetu Leo machi 25, 2026 Shinyanga – Matokeo ya uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) 2026/2027 yametangazwa, huku jumla ya kura 104 zikipigwa, ambapo kura 6 zimetajwa kuharibika. Kwa mujibu wa matokeo hayo, Maduhu ameongoza kwa kupata kura 43, akifuatiwa na Sharon aliyepata kura 21. Nafasi ya tatu imechukuliwa na Vicent kwa kura 16, huku Moris Daudi akipata kura 14 na Sitta Matias akipata kura 10. Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi imetoa muda wa wiki moja kwa wagombea au wanafunzi wenye malalamiko kuwasilisha pingamizi rasmi kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi huo. Malalamiko Yalianza Kujitokeza Baadhi ya wagombea kueleza kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo, wakidai kuwa haukuwa wa haki na usawa. Miongoni mwa hoja zilizotolewa ni pamoja na madai ya kuwepo kwa mkanganyiko wa sanduku la kura, ambapo inadaiwa kuwa sanduku hilo Lili ondoka Kwa mazingira ya kutatani hasa baada ya kumaliza kupiga kura huku ikielezwa wazi kuwa makampeni meneja Hawa kuhusiswa kuhusu uamzi huo ...

Mwl. Moris Daudi Afunga Kampeni Chuoni STJOSO: “Nitaanza na Haya”

Picha
  Na, Mwandishi wetu Chuoni  Leo, mgombea wa nafasi ya urais wa serikali ya wanafunzi wa ST. Joseph College (STJOSO) 2026/2027, Mwl. Moris Daudi, amefunga rasmi kampeni zake chuoni, akibeba kaulimbiu yake ya “ Mabadiliko Chanya ni Sasa” . Katika hotuba yake ya kufunga kampeni, Moris aliwahakikishia wanafunzi kwamba endapo atachaguliwa, ataanza na haya: “ Nitaanza na haya: Kuboresha computer lab na studio ya uandishi wa habari ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia. Kuimarisha huduma ya Wi-Fi chuoni, ili intaneti iwe ya haraka, thabiti na inafaa kwa masomo na utafiti. Kuangalia upya na kuboresha utaratibu wa tisheti za Jumatano na Ijumaa , kuhakikisha ubora unaowiana na mahitaji ya wanafunzi. Kuboresha mazingira ya hosteli kuwa salama, safi na rafiki – jambo ambalo bado linahitaji tathmini ya moja kwa moja. Kushughulikia changamoto za kiusafiri, kuhakikisha usafiri wa wanafunzi ni salama, wa haraka na unalingana na ratiba ya masomo.” Kwa upande wake ...

MWL. MORIS DAUDI AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO STJOSO 2026/2027

Picha
Picha: Mwalimu moris akizungumza  Na, milu malimi Leo machi 23, 2026 Mgombea wa nafasi ya urais wa serikali ya wanafunzi ST. Joseph College (STJOSO) kwa mwaka 2026/2027 , Mwl. Moris Daudi, amezindua kampeni zake kwa kishindo, akibeba kaulimbiu ya “ Mabadiliko Chanya ni Sasa ,” huku akiahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi chuoni hapo. Picha: Chanzo Thadeo Media library   Moris Daudi, anayefahamika kama mwanamichezo maarufu na mshiriki wa mashindano ya Miss na Mrs katika miaka ya 2024/2025 na 2025/2026 yakijulikana kama st Joseph talent , ameanza kampeni zake kwa mvuto mkubwa miongoni mwa wanafunzi. Mbali na umaarufu huo, pia anajulikana kwa moyo wake wa kujitolea, ucheshi wake, urafiki na wenzake, Picha mwl. Moris tour 2025/26 Akiwa na baadhi ya washiliki Chanzo Thadeo Media library  pamoja na uzoefu wa tour 2024/25   Picha Chanzo Thadeo Media library   pia Kwa moyo wake wa kujitolea kufundisha kufundisha Jomu  School Shinyan...