Mwl. Moris Daudi Afunga Kampeni Chuoni STJOSO: “Nitaanza na Haya”
Na, Mwandishi wetu Chuoni
Leo, mgombea wa nafasi ya urais wa serikali ya wanafunzi wa ST. Joseph College (STJOSO) 2026/2027, Mwl. Moris Daudi, amefunga rasmi kampeni zake chuoni, akibeba kaulimbiu yake ya “Mabadiliko Chanya ni Sasa”. Katika hotuba yake ya kufunga kampeni, Moris aliwahakikishia wanafunzi kwamba endapo atachaguliwa, ataanza na haya:
“Nitaanza na haya:
Kuboresha computer lab na studio ya uandishi wa habari ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia.
Kuimarisha huduma ya Wi-Fi chuoni, ili intaneti iwe ya haraka, thabiti na inafaa kwa masomo na utafiti.
Kuangalia upya na kuboresha utaratibu wa tisheti za Jumatano na Ijumaa, kuhakikisha ubora unaowiana na mahitaji ya wanafunzi.
Kuboresha mazingira ya hosteli kuwa salama, safi na rafiki – jambo ambalo bado linahitaji tathmini ya moja kwa moja.
Kushughulikia changamoto za kiusafiri, kuhakikisha usafiri wa wanafunzi ni salama, wa haraka na unalingana na ratiba ya masomo.”
Kwa upande wake, mgombea mwenza wa nafasi ya Makamu wa Rais, Maria Baraza, ameeleza kuwa atakazia zaidi mazingira bora ya hosteli, huduma za masomo, na usalama wa wanafunzi, akisisitiza kwamba maendeleo ya mwanafunzi yanahitaji kuanza na mazingira salama, rafiki na yenye kukidhi mahitaji muhimu.
Picha: Mbali mbali AKIWA na timu yake huku wakiguatilia changamoto Kwa ukalibu
Mwl. Moris, anayejulikana kwa umaarufu wake wa michezo, ucheshi, moyo wa kujitolea na urafiki, amesema timu yake tayari imeweza kutembelea sehemu zenye changamoto chuoni, ikiwa ni pamoja na computer lab na studio ya uandishi, ili kuona hali halisi ya changamoto za wanafunzi. Hata hivyo, kura zenu ni Mhimu
Uchaguzi wa STJOSO 2026/2027 unatarajiwa kufanyika kesho, Machi 25, 2026, ambapo wanafunzi wote watapata nafasi ya kuchagua viongozi wao wapya wa serikali ya wanafunzi. Uzinduzi na kufunga kampeni za Moris Daudi zimeonesha kuanza kwa ushindani mkali, huku kaulimbiu yake ya Mabadiliko Chanya ni Sasa”. matumaini ya maboresho dhahiri katika maisha ya wanafunzi chuoni.












Maoni
Chapisha Maoni