MWL. MORIS DAUDI AZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO STJOSO 2026/2027
![]() |
| Picha: Mwalimu moris akizungumza |
Na, milu malimi
Leo machi 23, 2026 Mgombea wa nafasi ya urais wa serikali ya wanafunzi ST. Joseph College (STJOSO) kwa mwaka 2026/2027, Mwl. Moris Daudi, amezindua kampeni zake kwa kishindo, akibeba kaulimbiu ya “Mabadiliko Chanya ni Sasa,” huku akiahidi kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi chuoni hapo.
![]() |
| Picha: Chanzo Thadeo Media library |
Moris Daudi, anayefahamika kama mwanamichezo maarufu na mshiriki wa mashindano ya Miss na Mrs katika miaka ya 2024/2025 na 2025/2026 yakijulikana kamast Joseph talent, ameanza kampeni zake kwa mvuto mkubwa miongoni mwa wanafunzi. Mbali na umaarufu huo, pia anajulikana kwa moyo wake wa kujitolea, ucheshi wake, urafiki na wenzake,
![]() |
| Picha mwl. Moris tour 2025/26 Akiwa na baadhi ya washiliki Chanzo Thadeo Media library |
pamoja na uzoefu wa tour 2024/25
![]() |
| Picha Chanzo Thadeo Media library |
![]() |
| Picha: mwl. Moris akizungumza Leo |
Katika uzinduzi huo wa kampeni, Moris alisema kuwa endapo atachaguliwa kuongoza serikali ya wanafunzi, ataanza na suala la uboreshaji wa miundombinu, hasa kwenye computer lab, kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kupata mazingira bora zaidi ya kujifunzia. Pia alitaja umuhimu wa kuboresha vifaa vya uandishi wa habari, huduma ya Wi-Fi, pamoja na kuangalia upya suala la tisheti za Jumatano na Ijumaa, ili ziwe na ubora na utaratibu unaoendana na mahitaji ya wanafunzi.
![]() |
| Picha: Maria Baraza |
Kwa upande wake, mgombea mwenza wa nafasi ya Makamu wa Rais, Maria Baraza, alisisitiza zaidi suala la hostel na haja ya kuwa na mazingira bora ya kujifunzia, akieleza kuwa maendeleo ya mwanafunzi yanahitaji kuanza na mazingira salama, rafiki na yenye kukidhi mahitaji muhimu.
![]() |
| Picha Mbali mwl. Moris akiwa na timj yake wakitembelea maeneo mbali mbali yenye changamoto |
Sambamba na uzinduzi huo, Moris Daudi na timu yake walifanikiwa kutembelea baadhi ya maeneo yenye changamoto chuoni hapo, yakiwemo computer lab na studio ya wanafunzi wa uandishi wa habari, Mazingira ya choooni na chumba Cha watu wa sekeletal hatua ambayo imeelezwa kuwa ni sehemu ya kujionea kwa karibu hali halisi ya changamoto zinazowakabili wanafunzi hao.
Katika kinyang’anyiro hicho, Moris Daudi anatarajiwa kukutana na ushindani kutoka kwa baadhi ya majina yanayotajwa kuwa na ushawishi ndani ya siasa za wanafunzi chuoni hapo. Miongoni mwao ni Sitta Matias, aliyewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria 2025/26, anayejulikana kwa nidhamu, upole na maadili ya hali ya juu. Pia anatajwa Mh. Vicent Chacha, rais wa awali wa mwaka 2025/26, anayefahamika kwa msimamo thabiti katika kutetea maslahi ya wanafunzi, pamoja na Raphael Elias, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge 2025/26.
![]() |
| Picha: Mbali mbali mwl. Moris akiwa Anafungua kampeni za urais STJOSO 2026/27 |
![]() |
Kwa ujumla, uzinduzi wa kampeni za Mwl. Moris Daudi umeonyesha kuanza kwa ushindani mkubwa wa uchaguzi wa STJOSO 2026/2027, huku kaulimbiu ya “Mabadiliko Chanya ni Sasa” ikiendelea kuwavutia wanafunzi wengi wanaotamani kuona maboresho ya kweli katika mazingira yao ya kujifunzia.
Samahani kwa changamoto yoyote. Blog yetu bado ipo katika hatua za mwisho za kudizaini. Endelea kufuatilia

































Maoni
Chapisha Maoni