MATOKEO YA UCHAGUZI STJOSO 2026/2027 YAZUA MJADALA
Na Mwandishi wetu
Leo machi 25, 2026 Shinyanga – Matokeo ya uchaguzi wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) 2026/2027 yametangazwa, huku jumla ya kura 104 zikipigwa, ambapo kura 6 zimetajwa kuharibika.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, Maduhu ameongoza kwa kupata kura 43, akifuatiwa na Sharon aliyepata kura 21. Nafasi ya tatu imechukuliwa na Vicent kwa kura 16, huku Moris Daudi akipata kura 14 na Sitta Matias akipata kura 10.
Hata hivyo, Tume ya Uchaguzi imetoa muda wa wiki moja kwa wagombea au wanafunzi wenye malalamiko kuwasilisha pingamizi rasmi kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi huo.
Malalamiko Yalianza Kujitokeza
Baadhi ya wagombea kueleza kutoridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo, wakidai kuwa haukuwa wa haki na usawa. Miongoni mwa hoja zilizotolewa ni pamoja na madai ya kuwepo kwa mkanganyiko wa sanduku la kura, ambapo inadaiwa kuwa sanduku hilo Lili ondoka Kwa mazingira ya kutatani hasa baada ya kumaliza kupiga kura huku ikielezwa wazi kuwa makampeni meneja Hawa kuhusiswa kuhusu uamzi huo kwa muda fulani bila maelezo ya kutosha, jambo lililozua maswali kuhusu usalama na uaminifu wa kura.
Wanafunzi, Baada ya matokeo kutangazwa, hali ya mjadala imeongezeka chuoni hapo huku wanafunzi wakionekana kugawanyika katika mitazamo tofauti.
Baadhi wamepongeza matokeo hayo wakisema yameakisi mapenzi ya wengi, huku wengine wakionesha kutoridhishwa wakidai kulikuwa na mapungufu katika mchakato wa uchaguzi.
Kwa upande wa, Tume ya Uchaguzi imeeleza kuwa haikupanga kutokea kwa hali hiyo, lakini imewahimiza wahusika wote wenye malalamiko kufuata taratibu rasmi za kuwasilisha pingamizi ndani ya muda uliotolewa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Maduhu Akizungumza
Baada ya kutangazwa kuongoza kwa kura nyingi, Maduhu aliwashukuru wapiga kura pamoja na wagombea wenzake kwa kushiriki katika mchakato huo. Hata hivyo, alikiri kuwepo kwa changamoto, akisema ni muhimu kwa wale wanaoona hawakuridhika kuwasilisha malalamiko yao ili haki iweze kutendeka.
Mchakato wa Uchaguzi Ulivyokuwa
Mchakato wa uchaguzi huo ulianza rasmi kwa zoezi la kuchukua fomu kuanzia tarehe 12 Machi hadi 16 Machi 2026.
Baada ya hapo, wagombea waliwasilisha fomu zao kati ya tarehe 17 hadi 18 Machi 2026, kabla ya kufanyika kwa mchujo (screening) tarehe 19 Machi 2026.
Kampeni rasmi zilianza tarehe 23 hadi 24 Machi 2026, ambapo wagombea waliwasilisha sera zao kwa wanafunzi, huku uchaguzi mkuu ukifanyika Leo tarehe 25 Machi 2026.
Kwa ujumla, Matokeo hayo yameacha mjadala mkubwa miongoni mwa wanafunzi wa STJOSO, huku macho yakielekezwa katika hatua ya pingamizi ambayo inaweza kuathiri hatima ya matokeo hayo endapo ushahidi wa kuridhisha utawasilishwa.


Maoni
Chapisha Maoni