𝐒𝐇𝐀𝐑𝐎𝐍 𝐀𝐀𝐏𝐈𝐒𝐇𝐖𝐀 𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐌𝐏𝐘𝐀 𝐒𝐓𝐉𝐎𝐒𝐎 2026/27, 𝐕𝐈𝐂𝐄𝐍𝐓 𝐀𝐓𝐎𝐀 𝐔𝐒𝐇𝐀𝐔𝐑𝐈 𝐌𝐙𝐈𝐓𝐎
Na Thadeo Gelema, Shinyanga
Leo Aprili 13, 2026 Rais mpya wa Serikali ya Wanafunzi (STJOSO) 2026/2027, Sharon Callist Mathias, ameapishwa rasmi kushika wadhifa huo, akiahidi kuanza kazi mara moja kwa kushughulikia changamoto zinazowakabili wanafunzi, ikiwemo suala la bima ya afya ambalo amelipa kipaumbele cha juu.
Hafla ya kuapishwa iliyofanyika chuoni hapo imehudhuriwa na viongozi wa chuo, wanafunzi pamoja na wageni mbalimbali, huku ikitawaliwa na matumaini mapya ya uongozi.
Akizungumza baada ya kula kiapo, Sharon alisema kuwa uongozi wake utaanza kwa kugusa mahitaji ya msingi ya wanafunzi.
“Kipaumbele changu cha kwanza ni kushughulikia changamoto ya bima ya afya kwa wanafunzi, pamoja na kuboresha upatikanaji wa vifaa vya makatibu na vifaa vya uandishi wa habari,” alisema Shaloni.
Aidha, alisisitiza kuwa ataimarisha mahusiano kati ya wanafunzi, walimu, serikali ya chuo pamoja na taasisi binafsi ili kujenga mazingira bora ya kujifunzia na kushirikiana.
Kwa upande wake, Rais mstaafu, Vicent Chacha, alimpongeza Shaloni kwa ushindi wake na kumtaka kuongoza kwa hekima, uvumilivu na ushirikiano.
Vicent alibainisha kuwa katika kipindi chake cha uongozi walifanya jitihada mbalimbali za kijamii, ikiwemo kusaidia watoto yatima, pamoja na kushughulikia baadhi ya changamoto za wanafunzi.
“Tulijitahidi si tu kushughulikia masuala ya ndani ya chuo, bali pia kugusa jamii kwa kusaidia makundi yenye uhitaji kama watoto yatima. Ni muhimu uongozi huu mpya kuendeleza moyo huo,” alisema Vicent.
Aliongeza kuwa uongozi ni dhamana inayohitaji kusikiliza wanafunzi na kushirikiana na wadau wote ili kuleta mabadiliko ya kweli.
Naye Mkurugenzi wa chuo hicho, Miraji Chomoka,
"alisema anatarajia kuona uongozi mpya ukiwa na ubunifu na matokeo chanya zaidi, akiahidi kutoa ushirikiano wa karibu kwa serikali ya wanafunzi".
Uchaguzi wa mwaka huu ulifanyika kwa marudio baada ya kuwepo kwa malalamiko katika awamu ya kwanza, hali iliyosababisha mabadiliko ya matokeo ambapo Sharon aliibuka mshindi kwa kupata kura 23 kati ya kura 49 zilizopigwa.
Kwa ujumla, wanafunzi wameonesha matumaini makubwa kwa uongozi huo mpya, wakiamini kuwa utaleta mabadiliko chanya na kuboresha mazingira ya kujifunzia pamoja na ustawi wa wanafunzi.
| Rais mpya wa STJOSO 2026/2027, Sharon (Shaloni), akihutubia wanafunzi jukwaani mara baada ya kuapishwa rasmi chuoni hapo. |
| Mkurugenzi wa chuo, Miraji Chomoka, akijibu hotuba wakati wa hafla ya kuapishwa kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi. |
| Makamu wa Rais wa STJOSO akila kiapo rasmi cha kuingia madarakani wakati wa hafla ya kuapishwa kwa viongozi wa serikali ya wanafunzi 2026/2027 chuoni hapo. |
| Rais Shaloni (katikati) akiwa na Makamu wa Rais pamoja na viongozi wengine wa STJOSO mara baada ya kula kiapo cha uongozi. |
| Rais mstaafu Vicent Chacha akizungumza jukwaani, akitoa ushauri na kueleza uzoefu wake wa uongozi kwa viongozi wapya. |

Maoni
Chapisha Maoni