RASIMISHENI NAMBA ZA USAJILI ZA VYOMBO VYA MOTO.
![]() |
| Picha: Sajenti David Ndimila wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga akitoa elimu kwa dereva |
Leo February 23, 2026 Madereva wa vyombo vya moto wametakiwa kufanya urasimishaji wa namba za usajili za vyombo hivyo pasipo shuruti mara baada ya kibali Cha muda mfupi kuisha.
Akitoa elimu hiyo Kwa madereva wa vyombo vya moto Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaeleza kuwa kuendesha vyombo vya moto Kwa kutumia namba ya chasi (chasiss number) bila namba ya usajili ni kosa kisheria mara baada ya muda wa kibali hicho Cha muda mfupi kuisha.
Sajenti Ndimila amewataka madereva hao kujisimamia na kutekeleza takwa la kisheria bila shuruti pindi wanapotoa vyombo hivyo bandarini au kuvinunua vikiwa na namba ya chasi (chassis number)
![]() |
![]() |
Kwa ujumla, Madereva wanahimizwa kurasimisha namba za usajili kwa wakati ili kuepuka adhabu na kuongeza usalama barabarani, kwani ni takwa la kisheria na wajibu wa kila mmiliki wa chombo cha moto.





Maoni
Chapisha Maoni