CHUKUA TAHADHALI KABLA YA KULIPITA GARI LINGINE

PICHA: Sajenti David Ndimila akitoa elimu ya usalama kwa madereva kuhusu namna sahihi ya kulipita gari barabarani




 
Hii ni Thadeo media

Leo February 26, 2026 Madereva wa magari makubwa yanayokwenda masafa marefu wamepatiwa elimu ya namna ya kujiepusha na ajali wanapotaka kuyapita magari mengine barabarani.

Elimu hiyo imetolewa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, ambaye amewataka madereva kujiridhisha kuwa hakuna hatari kwa watumiaji wengine wa barabara kabla ya kufanya uamuzi wa kulipita gari lililo mbele yao.

Amesisitiza kuwa kabla ya kulipita gari la mbele, dereva anatakiwa kuacha nafasi ya kutosha kati ya gari analoliendesha na lile lililo mbele yake ili aweze kuona kwa urahisi magari yanayokuja kutoka upande wa mbele, na hivyo kufanya maamuzi sahihi na salama.

PICHA: Mbali mbali Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, akitoa elimu kwa madereva wa magari makubwa yanayosafiri masafa marefu kuhusu namna sahihi ya kulipita gari lingine kwa kuacha nafasi ya kutosha na kujiridhisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara kabla ya kufanya uamuzi.


Kwa ujumla, madereva wametakiwa kuwa makini na kuchukua tahadhari wanapolipita gari lingine ili kulinda maisha yao na ya watumiaji wengine wa barabara.

Maoni

  1. 💯💯 Nikwel Kwan Hawa jamaa waga Wana jiangalia wao2

    JibuFuta

Chapisha Maoni