𝐂𝐇𝐔𝐊𝐔𝐄𝐍𝐈 𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐕𝐈𝐕𝐔𝐊𝐎 𝐕𝐘𝐀 𝐑𝐄𝐋𝐈

 Na, Thadeo Gelema 

Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu kuheshimu vivuko vya reli ili kuepuka ajali za mara Kwa mara.

Picha: Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti David Ndimila, akitoa elimu kwa maafisa usafirishaji (bodaboda) kuhusu umuhimu wa kuheshimu vivuko vya reli.

Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila katika kituo Cha Maafisa usafirishaji Cha Ally's star ambapo amewataka madereva hao kuheshimu vivuko vya reli Kwa kusimama na kujiridhisha hali ya kiusalama kabla ya kuchukua maamuzi ya kuvuka.

Picha: Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda wakimsikiliza kwa makini Sajenti David Ndimila wakati wa mafunzo ya usalama barabarani katika kituo cha Ally’s Star, Shinyanga.

Sajenti Ndimila amewaelimisha kwamba Treni inapaswa kupewa kipaumbele kwahiyo kila mmoja anawajibika kuheshimu vivuko hivyo kuepukana na ajali ambazo zinaweza kusababisha vifo, majeruhi na uharibifu baada ya kuigonga Treni.

Picha: Bodaboda wakielimishwa juu ya tahadhari za kuchukua kabla ya kuvuka reli ili kuepuka ajali na kulinda maisha yao pamoja na abiria.

Aidha,Maafisa usafirishaji hao wametakiwa kuwa mabalozi wa usalama barabarani Kwa kupaza sauti zao Kwa kuwaelimisha watumiaji wengine wa vyombo vya moto ili kutokomeza matukio ya ajali kwenye vivuko vya reli.

Picha: Maafisa usafirishaji wakitakiwa kuwa mabalozi wa usalama barabarani kwa kutoa elimu kwa watumiaji wengine wa vyombo vya moto kuhusu hatari za kupuuza vivuko vya reli.

Kwa ujumla, Ni wajibu wa kila dereva na mtumiaji wa barabara kuhakikisha anazingatia sheria na tahadhari zote, hususan kusimama na kujiridhisha usalama kabla ya kuvuka reli. Kwa kufanya hivyo, maisha yanaweza kuokolewa na ajali zisizo za lazima kuepukika.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀