𝐋𝐈𝐏𝐄𝐍𝐈 𝐓𝐎𝐙𝐎 𝐙𝐀 𝐌𝐀𝐊𝐎𝐒𝐀 𝐁𝐀𝐑𝐀𝐁𝐀𝐑𝐀𝐍𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐓𝐈
Hii ni Thadeo Media
Madereva wa Magari Mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu utii wa Sheria bila shuruti Kwa kulipa tozo zinazotokana na makosa ya usalama barabarani Kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kuzuiwa na kulipa madeni Kwa lazima pindi tozo hizo zinapokuwa zimeongezeka baada ya siku saba kuisha.
Picha: inaonesha askari wa usalama barabarani akifanya ukaguzi kwa dereva wa gari la mizigo lililosimama pembeni ya barabara.
Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaelimisha madereva hao kuwa faida ya kulipa tozo hizo mapema inarahisisha usimamizi wa Sheria, inasaidia kuepuka usumbufu mara Kwa mara pia kuepuka adhabu Kali zaidi
Picha: inaonesha askari wa usalama barabarani akiwa amesimama kando ya barabara akizungumza na dereva wa gari ndogo aina ya s
Takix.
Aidha, Sajenti Ndimila amewataka wamikiki wa Magari kuwa na tabia ya kukagua Magari yao pindi wanapotoka kuwapa watu wengine ili kujua kama yameandikiwa faini na kuweza kuwajurisha walioandikiwa faini wazilipe Kwa wakati.
Kwa ujumla, picha hizi zinaakisi operesheni ya usalama barabarani inayoendeshwa na Jeshi la Polisi mkoni Shinyanga
🔚 Kwa ujumla, elimu iliyotolewa kwa madereva mkoani Shinyanga inaonesha umuhimu wa kuwajibika na kufuata sheria za usalama barabarani bila kulazimishwa. Ulipaji wa tozo kwa wakati si tu unasaidia kuepuka usumbufu na gharama za ziada, bali pia unachangia katika kuimarisha nidhamu ya matumizi ya barabara.

Maoni
Chapisha Maoni