𝐃𝐂 𝐌𝐓𝐀𝐓𝐈𝐑𝐎 𝐌𝐀𝐑𝐔𝐅𝐔𝐊𝐔 𝐓𝐀𝐀𝐒𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐅𝐄𝐃𝐇𝐀 𝐊𝐔𝐅𝐈𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐌𝐀𝐋𝐈 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye kikao kuangalia namna ya kumaliza changamoto ya taasisi za fedha zinazonyanyasa wananchi wanapochelewa kurejesha mikopo wanakwenda kuwafilisi mali zao jambo ambalo linakiuka sheria kwani wao hawana mamlaka hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro ameanza kuchukuwa hatua kwa taasisi za fedha zinazokopesha fedha  kisha kwenda  kubeba vitu vya watu mtaani wanapokuwa wamechelewa kurejesha mikopo jambo ambalo ni kinyume cha sheria na taratibu.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatia kuenea kwa mikopo umiza maarufu kama kausha damu, inayotolewa na baadhi ya taasisi na watu binafsi kwa riba kubwa, huku wakopaji wakikumbwa na vitisho na mali zao kuchukuliwa  wanaposhindwa kurejesha kwa wakati.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro ametoa agizo wakati wa kikao na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za fedha,amesema vitendo vya kunyanyasa wananchi  havikubaliki na nilazima kuchukuwa hatua.

Amesisitiza kuwa ni marufuku kwa mkopeshaji yeyote kuchukua mali za mkopaji bila kufuata taratibu za kisheria, akibainisha kuwa njia sahihi ni kufungua shauri mahakamani ili kupata uamuzi halali.

 

Mwanasheria wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Rose Matunda, amesema wapo watu wanaojihusisha na utoaji mikopo bila kuwa na vibali halali, jambo linalochangia ukiukwaji wa sheria na unyonyaji kwa wananchi.

Amesema mikataba ya mikopo inapaswa kuwa wazi na rahisi kueleweka kwa pande zote, lakini mara nyingi wakopaji hawapewi nafasi ya kuelewa masharti kabla ya kusaini.

Alisisitiza umuhimu wa kuweka usimamizi madhubuti ili kuhakikisha mikopo inatolewa kwa kuzingatia sheria na haki za wananchi zinalindwa.

Kwa ujumla, hatua ya Julius Mtatiro inalenga kulinda haki za wananchi dhidi ya unyonyaji wa baadhi ya taasisi za fedha, kwa kusisitiza kufuata sheria na taratibu sahihi. Ni wito kwa uwajibikaji kwa wakopeshaji na ulinzi zaidi kwa wakopaji ili kuhakikisha haki na usawa vinazingatiwa.


Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Peres Kamugisha

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye kikao





Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀