𝐔𝐒𝐀𝐋𝐀𝐌𝐀 𝐁𝐀𝐑𝐀𝐁𝐀𝐑𝐀𝐍𝐈 𝐉𝐔𝐊𝐔𝐌𝐔 𝐋𝐀 𝐊𝐈𝐋𝐀 𝐌𝐓𝐔 – 𝐒𝐀𝐉𝐄𝐍𝐓𝐈 𝐍𝐃𝐈𝐌𝐈𝐋𝐀

Na, Thadeo Gelema 

Katika kipindi cha hivi karibuni, Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa lengo la kupunguza ajali na kuongeza uelewa wa matumizi sahihi ya barabara.

Miongoni mwa askari wanaoendelea kufanya kazi kubwa ya utoaji elimu hiyo ni Sajenti David Ndimila ambaye amekuwa mstari wa mbele kuelimisha makundi mbalimbali ya watumiaji wa barabara ikiwemo madereva, bodaboda, abiria, wanafunzi pamoja na wananchi kwa ujumla.

Kupitia kampeni mbalimbali za elimu, Sajenti Ndimila amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuheshimu sheria za usalama barabarani, kuacha mwendokasi, kutumia usafiri salama, kuheshimu vivuko vya watembea kwa miguu pamoja na kutoa taarifa za makosa ya usalama barabarani.

Miongoni mwa elimu alizozitoa ni pamoja na kuwataka madereva wa magari ya mizigo kuacha kuwaruhusu matingo kuendesha magari bila sifa za udereva, kuhimiza bodaboda kuheshimu misafara, kuwataka madereva kuchukua tahadhari wanapoyapita magari mengine pamoja na kuelimisha wananchi kuhusu hatari ya kupanda bajaji za mizigo.

Aidha, Sajenti Ndimila ameendelea kuhamasisha abiria kuwa mabalozi wa usalama barabarani kwa kukemea mwendokasi, kutoa taarifa za makosa ya barabarani na kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoweza kutokea safarini.

Kwa upande wa waendesha bodaboda, amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuvaa vifaa vya usalama, kuheshimu watumiaji wengine wa barabara na kuacha vitendo hatarishi kama kutoboa eksozi zinazotoa kelele na milipuko mikubwa.

Wananchi wengi wanaonekana kupongeza juhudi zinazofanywa na Jeshi la Polisi pamoja na Sajenti David Ndimila kwa kuendelea kuwafikia wananchi moja kwa moja na kuwapatia elimu inayosaidia kuokoa maisha yao.

Kwa ujumla, elimu hiyo inalenga kujenga jamii yenye uelewa wa sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali, vifo na majeruhi. “Usalama barabarani unaanza na mimi na wewe.”

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀