POLISI DAR WAKAMATA WEVYE MILIO MIKALI YA PIKIPIKI NA MAGARI
![]() |
| Picha hii ni ya mfano kwa madhumuni ya kuonesha tukio husika na sio tukio halisi lililotokea wakati wa kukamatwa kwa watuhumiwa. Chanzo: Thadeo Media Library Photo. |
Na, Thadeo Gelema
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kuendesha vyombo vya moto kwa kutoa milio mikali ya milipuko kinyume cha sheria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi iliyotolewa Machi 06, 2026, watuhumiwa hao wanadaiwa kuendesha magari na pikipiki zenye kelele kali zinazofanana na milipuko, hali inayosababisha usumbufu na hofu kwa wananchi pamoja na kukiuka Sheria ya Usalama Barabarani.
Watuhumiwa waliokamatwa ni Abdallah Masumbuko mkazi wa Tabata, Julius Dismas mkazi wa Mwananyamala, Salehe Ally mkazi wa Kijitonyama na Mohamed Rashid mkazi wa Magomeni. Wote wanashikiliwa na Polisi huku hatua zaidi za kisheria zikiendelea kuchukuliwa dhidi yao.
Kwa ujumla, Jeshi la Polisi limewahimiza watumiaji wote wa barabara, hususan waendesha vyombo vya moto, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka usumbufu na hatari kwa wananchi wengine.


Maoni
Chapisha Maoni