𝐌𝐒𝐈𝐏𝐀𝐍𝐃𝐄 𝐁𝐀𝐉𝐀𝐉𝐈 𝐙𝐀 𝐌𝐈𝐙𝐈𝐆𝐎 𝐌𝐔𝐄𝐍𝐃𝐀𝐏𝐎 𝐌𝐈𝐍𝐀𝐃𝐀𝐍𝐈
Na, mwandishi wetu Shinyanga
Abiria wanaosafiri kwenda minadani wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuacha kupanda Bajaji za mizingo ili kuepukana na ajali za mara Kwa mara barabarani.
Elimu hiyo imetolewa leo may 10, 2026 na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila katika barabara ya Old Shinyanga ambapo amewaeleza abiria kuwa Bajaji ya mizigo sio usafiri salama kwao na haina mazingira rafiki kulinda usalama wao hivyo kuacha tabia ya kupanda usafiri huo wa kubebea mizigo badala yake kutafuta usafiri unaoruhusiwa kubeba abiria.
Sajenti Ndimila amewaeleza abiria hao kuwa kupanda bajaji ya mizigo ni hatari sana na inaweza kusababisha madhara makubwa kwao pindi ajali inapotokea.
Aidha abiria hao wameaswa kujitambua na kuacha kurubuniwa kupanda katika usafiria huo kwani dereva wa chombo husika anaangalia maslahi binafsi na sio usalama wao.
![]() |
| Picha: Sajenti David Ndimila akizungumza na wananchi kuhusu matumizi sahihi ya usafiri barabarani. |

Kwa ujumla, elimu hiyo inalenga kuwajengea wananchi uelewa wa kuchagua usafiri salama na kuepuka kupanda bajaji za mizigo ili kupunguza ajali, majeruhi na kulinda maisha ya watumiaji wa barabara.


Maoni
Chapisha Maoni