MSIVUKE BARABARA MUONAPO MAGARI YA DHARURA YAKIPITA
![]() |
| Picha: Sajenti David Ndimila akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Nhelegani, Shinyanga |
Leo March 03, 2026 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nhelegani iliyopo mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kuepuka kuvuka barabara wanapoona magari ya dharura yakipita.
Akitoa elimu hiyo, askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, amesema kuwa magari ya dharura ni yale yanayotoa huduma za kuokoa maisha na kulinda usalama wa umma. Magari hayo ni pamoja na ya kubebea wagonjwa, zimamoto na polisi.
Amefafanua kuwa magari ya dharura hupaswa kuwa na ving’ora au taa za bluu na nyekundu zinazomulika ili yapatiwe kipaumbele barabarani.
Aidha, Sajenti Ndimila amewasisitiza wanafunzi hao kuongeza umakini wanapotaka kuvuka barabara. Hata wanapokuwa kwenye kivuko cha watembea kwa miguu, wanapaswa kutoa kipaumbele kwa magari ya dharura kupita kwanza.
![]() |
| Picha: Sajenti David Ndimila akitoa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Nhelegani mkoani Shinyanga kuhusu umuhimu wa kutovuka barabara wakati magari ya dharura yanapopita. |
Kwa ujumla, Wanafunzi wametakiwa kutovuka barabara magari ya dharura yanapopita ili kulinda maisha yao na kutoa kipaumbele kwa huduma za uokoaji.



Maoni
Chapisha Maoni