TUMIA IPASAVYO ALAMA YA PEMBETATU
![]() |
| Picha: Sajenti David Ndimila akiwafundisha madereva juu ya matumizi sahihi ya alama ya pembetatu kuzuia aja |
Leo March 01, 2026 Madereva wa magari ya kubeba abiria wamekumbushwa umuhimu wa kubeba na kutumia ipasavyo alama ya pembetatu ya tahadhari (reflective triangle) pindi gari linapopata hitilafu barabarani, ili kuzuia ajali na kulinda usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
Akizungumza na madereva hao, Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, amesema alama hiyo ni muhimu kwa kuwaonya madereva wengine kuhusu uwepo wa gari lililoharibika, ajali au hatari iliyo mbele yao.
Ameeleza kuwa alama ya pembetatu inapaswa kuwekwa nyuma ya gari lililopata hitilafu na wakati mwingine mbele, kulingana na mazingira ya barabara, ili ionekane kwa urahisi mchana na usiku.
Kwa mujibu wa Sajenti Ndimila, alama hiyo inatakiwa kuwekwa umbali wa mita 50 hadi 100 kutoka lilipo gari lililoharibika. Umbali wa mita 100 unapendekezwa katika barabara za mwendo kasi, huku mita 50 zikitumika katika barabara za mijini au maeneo yenye mwendo wa chini.
Kwa Ujumla, Amesisitiza kuwa uzingatiaji wa taratibu hizi ni hatua muhimu katika kupunguza ajali na kuimarisha usalama barabarani.

Maoni
Chapisha Maoni