𝐓𝐀𝐈𝐑𝐈 𝐂𝐇𝐀𝐊𝐀𝐕𝐔 𝐍𝐈 𝐂𝐇𝐀𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐉𝐀𝐋𝐈 𝐁𝐀𝐑𝐀𝐁𝐀𝐑𝐀𝐍𝐈


Na, Thadeo Gelema 

Kuendesha gari lenye tairi zilizochakaa kumetajwa kuwa Moja ya sababu kubwa zinazosababisha ajali za barabarani.

Picha: Sajenti Ndimila akitoa elimu kuhusu hatari ya tairi chakavu.

Akitoa elimu hiyo Kwa madereva wa Magari ya mizigo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaelimisha  madereva kuacha Kuendesha Magari yenye tairi chakavu kuepuka ajali barabarani kwani tairi hizo huweza kupasuka ghafla na kupoteza uelekeo, kuteleza na kushindwa kusimama Kwa wakati pia kushindwa kustahimili kwenye barabara zenye mashimo na mawe Kisha kupelekea ajali barabarani 

Picha: dereva akikumbushwa umuhimu wa ukaguzi wa tairi.

Sajenti Ndimila amewataka madereva hao kukagua Magari hayo kabla ya kuanza safari na kubadilisha tairi chakavu pindi wanapozibaini ili kuzuia ajali zisizo za lazima wawapo barabarani.

Picha: kwa ujumla Elimu ya usalama barabarani ikiendelea kutolewa kwa madereva ili kupunguza ajali na kulinda maisha ya watumiaji wa barabara.

Kwa ujumla, madereva wametakiwa kuzingatia usalama wa vyombo vyao kabla ya safari kwa kuhakikisha wanatumia tairi zilizo salama ili kupunguza ajali na kulinda maisha ya watumiaji wa barabara.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀