MAMELODI SUNDOWNS MABINGWA (CAF CHAMPIONS 2026)
Na,Thadeo Gelema Miamba ya soka kutoka Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns (Bafana Ba Style), imetawazwa rasmi kuwa Mabingwa wapya wa Afrika baada ya kulazimisha sare ya 1-1 ugenini dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco katika mchezo wa pili wa Fainali ya CAF Champions League uliopigwa Jumapili, Mei 24, 2026, kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah jijini Rabat. Kwa sare hiyo , Mamelodi Sundowns inayofundishwa na kocha Miguel Cardoso imetwaa ubingwa huo mkubwa zaidi ngazi ya klabu barani Afrika kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 (aggregate), kufuatia ushindi wao wa bao 1-0 walioupata katika mchezo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld jijini Pretoria. Dakika 90 za Moto Jijini Rabat: Katika mchezo huo wa marudiano uliopigwa mbele ya umati mkubwa wa mashabiki wa Morocco, wenyeji AS FAR walikuwa wa kwanza kupata bao la uongozi mnamo dakika ya 40 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa kwa usahihi na nahodha wao, Mohamed Hrimat, kufuatia faulu iliyofanywa ...