𝐔𝐖𝐀𝐍𝐉𝐀 𝐖𝐀 𝐉𝐀𝐌𝐇𝐔𝐑𝐈 𝐃𝐎𝐃𝐎𝐌𝐀 𝐖𝐀𝐅𝐔𝐍𝐆𝐈𝐖𝐀


Na, Thadeo Gelema 

 Leo 15, may 2026 Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungulia uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutumika kwa michezo ya Ligi baada ya kufanya marekebisho yaliyokidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.

Uwanja huo uliofungiwa kutokana na miundombinu yake kutofaa kutumika kama ilivyoainishwa kwenye masharti ya Kanuni ya Leseni za Klabu umekaguliwa na kukidhi vigezo vya Kikanuni baada ya marekebisho yaliyoelekezwa kufanyika.

Hata hivyo, TFF inaendelea kuzikumbusha klabu kuendelea kuboresha na kutunza miundombinu ya viwanja vyao vya nyumbani kwa kushirikiana na wamiliki kwa klabu ambazo hazimiliki viwanja, ili michezo ya Ligi ichezwe kwenye viwanja bora vinavyosaidia kuongeza ushindani na thamani ya Ligi.

Kwa ujumla, Hatua hiyo ya TFF ni ishara ya kuendelea kuboresha mazingira ya mpira wa miguu nchini, huku ikisisitiza umuhimu wa viwanja bora katika kukuza ushindani, usalama wa wachezaji na maendeleo ya Ligi kwa ujumla.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀