𝐌𝐄𝐓𝐀𝐂𝐇𝐀; 𝐍𝐀𝐎𝐌𝐁𝐀 𝐑𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐁𝐄𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐋𝐀 𝐔𝐅𝐔𝐍𝐃𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐒𝐇𝐀𝐁𝐈𝐊𝐈

Na,  Thadeo Gelema 

Golikipa wa Singida Black Stars, Metacha Mnata, ameomba radhi rasmi kwa viongozi, benchi la ufundi, na mashabiki wa klabu hiyo kufuatia sintofahamu iliyotokea katika mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga SC uliochezwa Mei 22, 2026, kwenye Uwanja wa KMC Mwenge, jijini Dar es Salaam.

​Katika mchezo huo ambao Singida Black Stars ilikubali kichapo cha mabao 3-0, kulijitokeza picha ya kutoridhishwa na maamuzi ya benchi la ufundi wakati wa mchezo, jambo lililotafsiriwa kama utovu wa nidhamu.

​Kauli ya Metacha Mnata:

​Kupitia taarifa yake, Metacha amekiri kuwa kilichotokea kilitokana na mihemko na presha kubwa ya mchezo, lakini hakuwa na nia mbaya:

"Klichotokea kilikuwa ni matokeo ya hisia za mchezo na presha ya ushindani, lakini haikuwa dhamira yangu kuonyesha utovu wa nidhamu wala kudharau maamuzi ya Benchi la Ufundi. Ninaiheshimu timu yangu, kocha wangu na maamuzi yote yanayofanywa kwa maslahi ya klabu."

​Ameongeza kuwa amejifunza kutokana na tukio hilo na anaahidi kuendelea kupambana kwa ajili ya timu kwa nidhamu, kujituma, na mshikamano mkubwa na wenzake.

​Hali ya Ushindani Ligi Kuu

​Kichapo hicho cha mabao 3-0 kimeiacha Singida Black Stars ikijipanga upya kurekebisha makosa ya kiufundi na kisaikolojia ili kurejea kwenye hali ya ushindi katika mechi zinazofuata, huku Yanga ikizidi kujichimbia kileleni.

Hali ya Ushindani Ligi Kuu

​Kichapo hicho cha mabao 3-0 kimeiacha Singida Black Stars ikijipanga upya kurekebisha makosa ya kiufundi na kisaikolojia ili kurejea kwenye hali ya ushindi katika mechi zinazofuata, huku Yanga ikizidi kujichimbia kileleni.

Kwa ujumla; Kitendo cha Metacha Mnata kukiri makosa na kuomba radhi kimeonyesha ukomavu wa kimichezo na kulinda nidhamu ya klabu. Sasa macho ya mashabiki wa Singida Black Stars yapo kwa Benchi la Ufundi kuona kama watamwanzisha tena langoni kwenye mechi inayofuata.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀