𝐀𝐑𝐒𝐄𝐍𝐀𝐋 𝐈𝐍𝐀 𝐒𝐔𝐁𝐈𝐑𝐈𝐀 𝐔𝐁𝐈𝐍𝐆𝐖𝐀 𝐋𝐄𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍 𝐂𝐈𝐓𝐘 ⚽🏆

Na, Thadeo Gelema 

Manchester City leo inashuka dimbani kuivaa AFC Bournemouth katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu England, huku City ikihitaji ushindi ili kuendelea kuweka presha kwa Arsenal kwenye mbio za ubingwa.

Bournemouth wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na morali kubwa baada ya kufanya vizuri katika michezo yao ya nyumbani msimu huu, huku wakisaka nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.

Kwa upande wa Arsenal, wanakaribia kutwaa taji lao la kwanza la EPL baada ya miaka 22 tangu mafanikio ya kikosi cha “Invincibles” cha msimu wa 2003/04 kilichomaliza ligi bila kupoteza mchezo hata mmoja.

Iwapo Manchester City watapoteza pointi katika mchezo wa leo, Arsenal watatangazwa rasmi mabingwa wa England. 🔥⚽



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀