𝐖𝐀𝐋𝐈𝐎 𝐌𝐂𝐇𝐎𝐊𝐀 𝐌𝐁𝐀𝐏𝐏É! 𝐙𝐀𝐈𝐃𝐈 𝐘𝐀 𝐌𝐈𝐋𝐈𝐎𝐍𝐈 30
Wimbi la mashabiki wanaotaka nyota wa Real Madrid, Kylian Mbappé, kuondolewa ndani ya klabu hiyo limeendelea kuongezeka, huku zaidi ya watu milioni 30 wakidaiwa kusaini ombi hilo mtandaoni.
Hatua hiyo imekuja kufuatia matokeo yasiyoridhisha ya hivi karibuni ya Real Madrid, ambapo taarifa zinaeleza kuwa timu hiyo imepata ushindi mmoja pekee katika mechi sita za mwisho alizocheza Mbappé.
Aidha, baadhi ya wachambuzi wa soka wamebainisha kuwa Madrid imeonekana kufanya vizuri zaidi katika baadhi ya michezo ambayo mshambuliaji huyo hakuhusika.
Hata hivyo, mjadala mkubwa umeendelea mtandaoni huku wadau wengine wakidai kuwa sehemu ya waliosaini ombi hilo huenda si mashabiki halisi wa Madrid, bali ni watu kutoka nje wanaochochea mjadala huo.
👉 Soma zaidi: @thadeomedia5.blogspot.com

Maoni
Chapisha Maoni