TAIFA STARS YAPATIWA KITITA CHA MILIONI 500 BAADA YA KUTINGA 16 BORA AFCON


Na,Thadeo Gelema 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameizawadia timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) shilingi milioni 500 kufuatia kufanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora katika michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON).

Taarifa hiyo imetolewa leo Januari 03, 2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Taifa Stars kwa njia ya simu.

Waziri Mkuu Dkt. Nchemba amesema kuwa, Mheshimiwa Rais  amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi pamoja na Watanzania wote kwa mafanikio hayo ya kihistoria na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono timu hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Rais Dkt. Samia ameahidi kutoa zawadi nono zaidi endapo Taifa Stars itaendelea kufanya vizuri na kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo inayoendelea nchini Morocco. 🇲🇦

Zawadi hiyo ya shilingi milioni 500 ni ishara ya kutambua na kuthamini jitihada za Taifa Stars, huku ikiongeza morali kwa wachezaji kuendelea kupigania heshima ya Taifa na kuandika historia zaidi katika michuano ya AFCON inayoendelea nchini Morocco. 🇹🇿⚽

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀