𝐇𝐈𝐒𝐓𝐎𝐑𝐈𝐀 𝐘𝐀𝐕𝐔𝐍𝐉𝐈𝐊𝐀: 𝐀𝐋 𝐀𝐇𝐋𝐘 𝐊𝐎𝐌𝐁𝐄 𝐋𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈𝐒𝐇𝐎 𝐌𝐒𝐈𝐌𝐔 𝐔𝐉𝐀𝐎


Na,  Thadeo Gelema 

Mizani ya soka nchini Misri imepinduka! Miamba ya soka barani Afrika, Klabu ya Al Ahly, itakosekana kwenye michuano ya CAF Champions League msimu ujao kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya miaka 23, baada ya kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Misri.

​Waangukia Shirikisho
​Matokeo hayo yanaifanya Al Ahly kushuka na kushiriki Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) msimu ujao.

​Wakati Al Ahly wakiangukia huko, mahasimu wao wakubwa Zamalek wametwaa ubingwa wa ligi hiyo na kukata tiketi ya CAF Champions League, wakisindikizwa na Pyramids FC waliomaliza nafasi ya pili.

Historia ya Miaka 23 Yavunjika
​Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Capital Digital, mara ya mwisho kwa Al Ahly kukosekana kwenye michuano ya CAF Champions League ilikuwa ni mwaka 2003, kabla ya kuanza mfululizo wa kushiri michuano hiyo mikubwa ngazi ya klabu tangu msimu wa 2004.

Kwa ujumla, Al Ahly kushuka hadi Kombe la Shirikisho baada ya miaka 23 ni pigo kubwa linaloashiria mabadiliko makubwa ya nguvu ya soka nchini Misri msimu huu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀