Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Siasa

Siasa

Picha
 Wananchi Wa Jimbo JIpya la Itwangi Wajitokeza kwa wingi Kumuunga Mkono Ng. Azza Hillal  Itwangi, Shinyanga – Septemba 13, 2025: Maelfu ya wananchi wa Jimbo la Itwangi wamejitokeza leo kwenye uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, wakionesha kundi la imani na mahaba kwa Mgombea Ubunge wa CCM, Mhe. Azza Hillal Hamad, na kuahidi kumpa kura za ushindi Oktoba 29. Uzinduzi huo umehudhuriwa na wanachama wa CCM, wagombea udiwani, na viongozi wa ngazi mbalimbali, huku Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC), Munde Tambwe Abdalla, akiwa mgeni rasmi. Munde alimsifu Azza kuwa “Mbunge Jembe” mwenye ujasiri, uelewa wa masuala ya wananchi na uwezo wa kuleta maendeleo. Akizungumza na wananchi, Azza Hillal Hamad aliahidi kupeleka miradi ya maendeleo kwenye sekta za maji, elimu, afya na umwagiliaji, akisisitiza kukamilisha skimu za Nyida na miradi ya maji ya Ziwa Victoria na Tinde Package. Pia alimpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo SGR, baraba...

Siasa

Picha
 BALOZI DKT. NCHIMBI ALIVYO TIKISA KAMPENI KAHAMA, WABUNGE WAMPA NGUVU YA HOJA Kahama, Shinyanga – Septemba 4, 2025 Mgombea mwenza wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo alifanya ziara ya kampeni katika Wilaya ya Kahama, akihutubia mamia ya wananchi katika maeneo ya Isaka, Kagongwa, na Ushetu. Katika hotuba zake, Dkt. Nchimbi alisisitiza umuhimu wa amani, mshikamano, na maendeleo endelevu, huku akihimiza wananchi kuendelea kushirikiana na viongozi wa CCM katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 🗳️Ushirikiano wa Wabunge Wabunge wa mkoa wa Shinyanga walihudhuria kampeni hiyo, wakimpa Dkt. Nchimbi nguvu ya hoja kwa kueleza mafanikio ya CCM katika mikoa yao na kuhimiza wananchi kuendelea kuunga mkono chama hicho. Benjamin Lukubha Ngayiwa – Jimbo la Kahama Mjini Mabula J. Magangila – Jimbo la Msalala Emmanuel Peter Cherehani – Jimbo la Ushetu Wabunge hawa walisisitiza kuwa uwepo wa Dkt. Nchimbi unaonyesha jinsi chama kinavyowajali wananchi na ku...

Siasa

Picha
MGOMBEA URAIS KUPITIA CUF ATUA SHINYANGA, ANADI SERA KUELEKEA IKULU Thadeo media  MGOMBEA urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo, amewasihi wananchi wa Shinyanga kukipa kura nyingi chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 akiahidi kuwaletea maendeleo ya kweli. Amenadi sera hizo leo Septemba 4,2025 kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika eneo la stendi ya mabasi ya Wilaya ya Shinyanga Mjini. Gombo ameahidi iwapo Watanzania watampatia ridhaa ya kuingia Ikulu, hatua ya kwanza atakayochukua ni kumtoa gerezani Tundu Lissu ili awe huru na kusimamia mchakato wa Katiba Mpya ambayo amesema ni kilio cha wananchi wengi. Pia ameahidi kufuta gharama zote za matibabu, kutoa elimu bure kuanzia awali hadi chuo kikuu, pamoja na kufuta kikokotoo cha pensheni. Vilevile amesema serikali ya CUF itapitia upya mikataba yote yenye utata ikiwamo ya bandari ili kuhakikisha rasilimali za taifa zinawanufaisha wananchi. “Naombeni sana wananchi wa Shinyanga siku ya uchaguz...

Magazeti

Picha
 BALOZI DKT. NCHIMBI AZINDUA KAMPENI SHINYANGA  MAJIMBO  YA KISHAPU, SHINYANGA MJINI, SOLWA, ITWANGI RATIBA YA KESHO ISAKA NA KAHAMA Shinyanga, Septemba 3, 2025 – Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameongoza mkutano mkubwa wa kampeni leo katika majimbo ya Kishapu na Shinyanga Mjini. Maelfu ya wananchi walihudhuria miutano hiyo, wakiwa tayari kusikia mpango wa chama kwa uchaguzi ujao. Katika mkutano huo, Dkt. Nchimbi aliwahimiza wananchi kuendelea kuiunga mkono CCM na wagombea wake wa ubunge na udiwani. Wagombea walioahidiwa kuungwa mkono ni: Mhe. Patrobas Katambi – Shinyanga Mjini Mhe. Lucy Mayenga – Kishapu Mhe. Ahmed Salum – Solwa Mhe. Azza Hillal Hamad – Itwangi Wabunge hao pia walizungumza kwa ufupi, wakieleza utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika majimbo yao, ikiwemo ujenzi wa barabara, masoko, shule, vituo vya afya, na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Ibadakuli. Kwa mujibu wa ratiba ya kampeni iliyothibitis...

siasa

Picha
  Kipenga cha Kampeni za Uchaguzi Mkuu Tanzania 2025 Kimepulizwa Rasmi Leo 28 Agosti Na Thadeo Gelema Dar es Salaam, 28 Agosti 2025 – Uzinduzi rasmi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 umefanyika leo, huku vyama vya siasa vikijiandaa kwa mashindano makali kuelekea uchaguzi utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025 . Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ( NEC ) Ilisisitiza kuwa vyama vyote vya siasa vitapata haki ya kufanya kampeni kwa mujibu wa ratiba itakayowekwa na kamati za ngazi zote za uchaguzi. NEC Yahakikisha Uwanja Sawa Mwenyekiti wa NEC, Jaji  Jacobs  Mwambegele , amesisitiza umuhimu wa kampeni za kistaarabu na amani, akiwataka viongozi wa vyama kuhakikisha wafuasi wao wanazingatia sheria na kanuni za uchaguzi. Aidha, amewaahidi wagombea wote wenye sifa kupata fomu na kuteuliwa pale watakapotimiza masharti ya uteuzi. Uzinduzi wa Kampeni za Vyama Vikuu CCM (Chama Cha Mapinduzi): Rais Samia Suluhu Hassan amepitishwa kugombea muhula wake wa pili a...

Siasa

Picha
 Baba Levo  Kugombea Ubunge Kigoma Mjini Na Thadeo Gelema  Kigoma, Agosti 23, 2025 – Clayton Revocatus Chiponda maarufu kama Baba Levo ameteuliwa rasmi kugombea Ubunge katika Jimbo la Kigoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Taarifa ya uteuzi huo ilitangazwa jana na viongozi wa CCM, ikibainisha kuwa Baba Levo amepokea uteuzi huo kwa furaha na shukrani kwa imani iliyowekwa kwake. Akizungumza mara baada ya uteuzi, Baba Levo alisema kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa Kigoma Mjini na kuleta maendeleo endelevu katika jimbo hilo. Baba Levo amehamasisha wananchi wa Kigoma Mjini kushirikiana naye katika kufanikisha miradi ya maendeleo na kuhakikisha kuwa kila raia anapata fursa sawa. Kwa sasa anajiandaa kuanza kampeni rasmi za uchaguzi, huku akilenga kuimarisha huduma za jamii na maendeleo ya kiuchumi. Hii ni fursa mpya kwa wananchi wa Kigoma Mjini kuhoji na kujadili hoja zinazohusu maendeleo ya jimbo lao kabla ya uchaguzi mkuu uja...

Siasa

Picha
 Dkt. Asha-Rose Migiro Ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Mwanamke wa Kwanza Kushika Wadhifa Huu Na Thadeo Gelema  Agosti 23, 2025 Dodoma Tanzania – Dkt. Asha-Rose Migiro ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akichukua nafasi ya Dkt. Emmanuel Nchimbi, na kuandika historia kama mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huu. Dkt. Migiro ni mwanasiasa namwanadiplomasia mwenye uzoefu mkubwa wa kitaifa na kimataifa. Kabla ya uteuzi huu, alihudumu katika nafasi kadhaa muhimu serikalini, ikiwa ni pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto (2000–2005), na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (2006–2007). Aidha, Dkt. Migiro aliteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (2007–2012), na baadaye akawa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza (2016–2023), ikionesha sifa zake za uongozi na diplomasia. Uteuzi wake kama Katibu Mkuu wa CCM unaashiria imani ya chama katika uongozi wake na ni pigo kubwa la kihistoria kwa usawa wa kijinsia katika si...

Siasa

Picha
 Kenani Kihongosi Amrithi Amos Makalla Kama Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Na Thadeo Gelema  Dodoma, Tanzania – Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya mabadiliko makubwa ya uongozi, ikimteua Kenani Kihongosi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, akichukua nafasi ya Amos Makalla. Uteuzi huu ulitangazwa Jumamosi, Agosti 23, 2025, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jijini Dodoma, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa chama, Rais Samia Suluhu Hassan. Kenani Kihongosi ni kiongozi kijana mwenye uzoefu mkubwa wa utumishi wa umma, akiihudumu CCM katika nafasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba na baadaye Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Uteuzi wake unaashiria mpango wa chama kuimarisha uongozi na kuhakikisha mafunzo bora ya wanachama katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025. Kwa upande mwingine, Amos Makalla, ambaye alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, ameondolewa katika nafasi hiyo. Taarifa rasmi kuhusu s...

Siasa

Picha
 Wagombea Ubunge CCM Mkoa wa Shinyanga 2025 Waliokubaliwa Rasmi Agosti 23, 2025 Thadeo media  Orodha ya Wagombea  1. Lucy Mayenga – Kishapu 2. Patrobas Katambi – Shinyanga Mjini 3. Emmanuel Cherehani – Ushetu 4. Azza Hillal Hamad – Itwangi 5. Ahmed Salum – Solwa 6. Mabula J. Magangila – Msalala 7. Benjamin Lukubha Ngayiwa – Kahama Mjini

Siasa

Picha
 Kura za Maoni CCM Kahama: Lukubha, Magangila na Cherehani Watingisha Majimbo ya Msalala, Kahama Mjini na Ushetu Na Mwandishi Wetu – Kahama, Agosti 5 Katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, Benjamin Lukubha Ngaiwa aliibuka mshindi kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini, baada ya kupata kura 2,093, akiwashinda wagombea wengine sita. Benjamin Lukubha Ngaiwa Aliyeshika nafasi ya pili alikuwa Sweetbert Charles Nkuba aliyepata kura 1,389, akifuatiwa na Jumanne Kibela Kishimba aliyepata kura 1,144. Wengine waliopata kura ni: Francis Fikili Mihayo – kura 821 Juliana Kajala Pallangyo – kura 256 James Daudi Lembeli – kura 219 David Anyandwile Kilala – kura 191 Kwa upande wa Jimbo la Msalala, jumla ya kura 7,845 zilipigwa ambapo kura 7,685 zilikuwa halali na 160 ziliharibika. Katika matokeo hayo, Mabula J. Magangila aliongoza kwa kura 5,518, akifuatiwa na: Mabula J. Magangila Ambrose N. Nakale – kura 929 Ezekiel Maige – kura 791 Simon Jame...

Siasa

Picha
 Lucy Mayenga Aliibuka Mshindi Kura za Maoni CCM Jimbo la Kishapu Na Mwandishi Wetu – Thadeo Gelema, Agosti 5 Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lucy Mayenga, aliibuka mshindi wa kura za maoni ndani ya chama hicho kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Kishapu, baada ya kupata kura 7,814 kati ya kura halali 12,864, hivyo kuwaacha wapinzani wake kwa tofauti kubwa. Bonda Nkinga alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,730, akifuatiwa na Bonophase Butondo, aliyemaliza muda wake wa ubunge, aliyepata kura 1,290. Wagombea wengine waliopata kura ni: Doto Kwigema – kura 597 George Jimisha – kura 590 Madaha Chaba – kura 503 John Ngano – kura 432 Jumla ya kura 18,443 zilipigwa katika mchakato huo wa kura za maoni, ambapo kura 201 ziliharibika. Ushindi wa Lucy Mayenga uliashiria uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wanachama wa CCM katika jimbo hilo, ambao waliamua kumpa nafasi ya kuongoza tena, safari hii wakimtaka agombee ubunge wa kuchaguliwa. Hata ...

Siasa

Picha
 Kura za Maoni CCM Itwangi: Azza Hillal Atikisa, Aliibuka Kidedea Na Mwandishi Wetu – Thadeo Gelema , Agosti 5 Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa zamani wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Azza Hillal Hamad, aliibuka kidedea na atikisa kura za maoni za CCM zilizofanyika jana, tarehe 4 Agosti 2025, katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini, kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo jipya la Itwangi. Katika kura hizo za maoni, Azza alipata kura 2,630 kati ya kura 5,580 zilizopigwa, huku kura halali zikiwa 5,551 na kura zilizoharibika 29. Azza aliwashinda wapinzani wake saba, huku John Elias Ntalimbo akiwa wa pili kwa kupata kura 2,322. Wagombea wengine ni Sebastian Pastory Malunde (kura 377), Fred Romanus Sanga (122), Chrispine Myeke Simon (45), Christian Misobi Budoya (28), Anna James Ng’wagi (16), na Hellena Daudi Mbuli (11). Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Erenestina Richard, alisema kuwa matokeo hayo ni ya awali na siyo uteuzi rasmi. “Kuongoza katika...

Siasa

Picha
 Ahmed Salum Aliongoza Kura za Maoni CCM Jimbo la Solwa Na Mwandishi Wetu – Thadeo Gelema, Agosti 5 Mbunge wa zamani wa Jimbo la Solwa, Ahmed Ally Salum, aliongoza kwa kishindo kura za maoni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika tarehe 4 Agosti 2025 katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini. Katika kura hizo, Salum alipata kura 3,862 kati ya kura halali 7,012 zilizopigwa, huku hakuna kura iliyoharibika. Aliongoza kwa tofauti kubwa dhidi ya wagombea wengine sita waliokuwa wakichuana naye kwenye mchakato huo wa ndani ya chama. Aliyeshika nafasi ya pili alikuwa Sosthenes Julius Katwale aliyepata kura 2,288. Wengine waliopata kura ni Selemani Emmanuel Chokala (645), Zinguji Mayala Machwele (67), Alphistone Michael Bushi (61), Costantine Joseph Budaga (59), na Leonard Nduta Lukanya aliyepata kura 30 pekee. Matokeo hayo yalitangazwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bi Erenestina Richard. Hata hivyo, alifafanua kuwa ushindi huo si uteuzi r...

Siasa

Picha
  Home SIASA KURA ZA MAONI CCM: TAZAMA HAPA WABUNGE WALIOONGOZA KWENYE MAJIMBO YAO Misalaba Media August 04, 2025 TAZAMA HAPA BAADHI YA WABUNGE WALIOONGOZA KURA ZA MAONI KWENYE MAJIMBO YAO