Siasa

 Kura za Maoni CCM Kahama: Lukubha, Magangila na Cherehani Watingisha Majimbo ya Msalala, Kahama Mjini na Ushetu

Na Mwandishi Wetu – Kahama, Agosti 5

Katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kahama, Benjamin Lukubha Ngaiwa aliibuka mshindi kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Kahama Mjini, baada ya kupata kura 2,093, akiwashinda wagombea wengine sita.

Benjamin Lukubha Ngaiwa

Aliyeshika nafasi ya pili alikuwa Sweetbert Charles Nkuba aliyepata kura 1,389, akifuatiwa na Jumanne Kibela Kishimba aliyepata kura 1,144. Wengine waliopata kura ni:

Francis Fikili Mihayo – kura 821

Juliana Kajala Pallangyo – kura 256

James Daudi Lembeli – kura 219

David Anyandwile Kilala – kura 191

Kwa upande wa Jimbo la Msalala, jumla ya kura 7,845 zilipigwa ambapo kura 7,685 zilikuwa halali na 160 ziliharibika. Katika matokeo hayo, Mabula J. Magangila aliongoza kwa kura 5,518, akifuatiwa na:

Mabula J. Magangila

Ambrose N. Nakale – kura 929

Ezekiel Maige – kura 791

Simon James Lufega – kura 189

Edson Simba Masondole – kura 152

Ramadhani Shiganza – kura 105

Wakati huo huo, katika Jimbo la Ushetu, CCM Wilaya ya Kahama ilimtangaza Emmanuel Peter Cherehani kuongoza katika matokeo ya awali, akipata kura 5,656. Hata hivyo, matokeo ya mwisho yalikuwa yakisubiriwa kutokana na marudio ya uchaguzi katika kata za Ubagwe, Mapamba na Bulungwa kufuatia malalamiko ya baadhi ya wanachama.

Emmanuel Peter Cherehani

Wagombea wengine katika jimbo hilo walipata kura zifuatazo:

Valelia Wilson Mwampashe – kura 153

Machibya Mwambilija Dofu – kura 171

Mussa Shilanga Misungwi – kura 452

Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga, aliwataka wanachama wote na wagombea kuwa watulivu, wakisubiri kwa subira na nidhamu maamuzi ya vikao vya juu vya chama, akisisitiza kuwa CCM inaongozwa na misingi ya haki, ustaarabu na maadili.

Kwa taarifa zaidi za kisiasa na maendeleo ya uchaguzi ndani ya CCM, tembelea daima Thadeo Media

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

𝐁𝐑𝐄𝐀𝐊𝐈𝐍𝐆 𝐍𝐄𝐖𝐒: 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐌𝐄𝐅𝐀𝐍𝐘𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀