Siasa

 Lucy Mayenga Aliibuka Mshindi Kura za Maoni CCM Jimbo la Kishapu

Na Mwandishi Wetu – Thadeo Gelema, Agosti 5

Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lucy Mayenga, aliibuka mshindi wa kura za maoni ndani ya chama hicho kwa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Kishapu, baada ya kupata kura 7,814 kati ya kura halali 12,864, hivyo kuwaacha wapinzani wake kwa tofauti kubwa.

Bonda Nkinga alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,730, akifuatiwa na Bonophase Butondo, aliyemaliza muda wake wa ubunge, aliyepata kura 1,290.

Wagombea wengine waliopata kura ni:

Doto Kwigema – kura 597

George Jimisha – kura 590

Madaha Chaba – kura 503

John Ngano – kura 432

Jumla ya kura 18,443 zilipigwa katika mchakato huo wa kura za maoni, ambapo kura 201 ziliharibika.

Ushindi wa Lucy Mayenga uliashiria uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wanachama wa CCM katika jimbo hilo, ambao waliamua kumpa nafasi ya kuongoza tena, safari hii wakimtaka agombee ubunge wa kuchaguliwa.

Hata hivyo, matokeo haya ni ya awali na uteuzi rasmi wa mgombea bado unategemea maamuzi ya vikao vya juu vya CCM, kama ilivyo desturi ya chama hicho.

Kwa taarifa zaidi kuhusu mchakato wa kisiasa Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla, endelea kutembelea Thadeo Media

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

BREAKING: RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MBALIMBALI

𝐓𝐀𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐈: 𝐏𝐎𝐋𝐈𝐒𝐈 𝐖𝐀𝐊𝐀𝐍𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐔𝐕𝐔𝐌𝐈 𝐌𝐖𝐀𝐍𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐈 𝐔𝐃𝐎𝐌 𝐊𝐔𝐖𝐀𝐖𝐀

𝐌𝐖𝐈𝐍𝐘𝐈; 𝐒𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐈𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐔𝐎𝐍𝐆𝐄𝐙𝐀 𝐌𝐃𝐀 𝐖𝐀 𝐔𝐑𝐀𝐈𝐒